SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, June 24, 2015

JANUARI MAKAMBA ATUA BUKOBA LEO, APATA MAPOKEZI MAKUBWA NA KUZOA WADHAMINI LUKUKI

Mh. January Makamba na mkewe, Ramona Makamba(kulia) baada ya kuwasili mkoani hapa Kagera kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho cha CCM. 
Picha na Faustine Ruta, Bukoba. Mh. January Makamba na mkewe, Ramona(kulia) mara baada ya kushuka kwenye Ndege leo hii Jumatano asubuhi juni 24, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba. Mh. January Makamba akisalimiana na Katibu wa Vijana Mkoa wa Kagera Mh. January Makamba akisalimiana na Wanafunzi wa Sekondari waliokuwa Uwanjani hapo ambao bila Shaka walikuwa wanasoma masomo ya Ndege inavyoruka na kutua na mengineyo kiujumla leo jumatano juni 24, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba Mh. January Makamba akisaini kwenye kitabu cha Wageni kwenye Uwanja Ndege Bukoba. Mh. January Makamba na mkewe, Ramona wakiteta jambo kwa furaha. Msafara wa Bodaboda kuelekea Mjini kwenye mzunguko na kugeuka kwenye Makao makuu ya CCM Mkoa wa Kagera
Mjini Bukoba, Bodaboda wakimsindikiza Mh. Januari Makamba Makamba akisalimia Wakazi wa Mji wa Bukoba walijitokeza kwa wingi January Makamba ameendelea na Ziara yake ya Kusaka Wadhamini katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania na leo hii jumatano juni 24, 2015 yupo hapa Mkoani Kagera akiomba Uzamini. Mh. January Makamba amepokelewa na wakazi wengi wa Mkoa wa Kagera wakiwemo Vijana walijitokeza kwa wingi kumpokea. Picha na Faustine Ruta, Bukoba Mh. Januari Makamba baada ya kusalimiana na Wakazi waliojitokeza kwenye Makao makuu ya CCM ameelekea katika Hospitali ya Mkoa kuwaona wagonjwa mbalimbali na Baada ya hapo ameelekea Wilayani Misenyi kwenda kusalimia Wakazi wa huko na Kuwaomba wamdhamini kwa kuweka saini fomu zake za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho cha CCM. Mh. Januari Makamba Akitia saini Katika kitabu cha wageni Ofisi za CCM January Akizungumza na wakazi wa Bukoba waliojitokeza kumsikiliza katika katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kagera leo Wakazi wa Mji wa Bukoba wakimsikiliza Mh. January Makamba kwa makini leo hii jumatano.

0 comments:

Post a Comment