SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, November 3, 2013

Matokeo Ya Mtihani Wa Darasa La Saba 2013

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

PSLE-2013 EXAMINATION RESULTS 
Imeelezwa kuwa ufaulu wa mtihani wa kumaliza darasa la  
 saba kwa mwaka 2013 umepanda kwa masomo yote kwa asilimia
19.89 ikilinganishwa na ilivyokuwa kwa mwaka uliopita.
Kwamba, wakati mwaka jana wahitimu waliopata asilimia
100 walikuwa asilimia 30.72, mwaka huu wameongezeka kuwa
asilimia 50.61. Pia, somo ambalo watahiniwa hao wamefaulu
zaidi katika mtihani wao ni  Kiswahili ambapo ufaulu ni
asilimia 69.06 huku wakiwa wamefeli zaidi kwenye somo la
Hisabati ambalo ufaulu upo chini kwa asilimia 28.62.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA),
Dk. Charles Msonde alisema wanafunzi 427,606
walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka
2013 huku kiwango cha udanganyifu kikizidi kudhibitiwa
hivyo kupungua.
Alisema NECTA imefuta matokeo yote ya mtihani wa kumaliza
elimu ya msingi kwa watahiniwa 13, ambao walibainika
kufanya udanganyifu kwenye mtihani au kurudia pasipo ruhusa ya Baraza. Watahiniwa waliofutiwa mwaka jana ni 293.
Alisema kati ya wanafunzi hao, 844,938 waliofanya mtihani
huo wamepata alama zaidi ya 100 katika alama 250:
“Idadi hiyo ni sawa na asilimia 50.61. Kati yao wasichana
walikuwa 208,227 (sawa na asilimia 46.68) na wavulana 219,379
sawa na asilimia 55.01,” alisema.
 Dk. Msonde alisema katika ufanyaji wa mtihani huo,
pia walikuwepo watu wenye ulemavu, ambapo wasichana
walikuwa 219 na wavulana 257.
Alisema matokeo hayo yatapelekwa maeneo yote husika
ili mchakato wa upangaji shule ukifanyika kwa watahiniwa
wote waliofaulu mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi.
Kuhusu usahihishaji mitihani, Dk. Msonde alisema ili kujiridhisha
 na usahihi wa zoezi la usahihishaji wa kutumia mfumo wa kompyuta
 (Optical Mark Reader - OMR), sampuli za karatasi 20,795 za
majibu ya watahiniwa wa shule 200 kutoka wilaya 48
zilichukuliwa kutoka shule za mikoa tisa ya (Iringa, Kagera,
Shinyanga, Manyara, Njombe, Mbeya, Morogoro, Katavi na Tanga)
na kusahihishwa kwa mkono: “Ulinganifu baina ya alama
za watahiniwa zilizopatikana kwa kusahihishwa kwa
mkono na zile zilizotokana na usahihishaji wa mfumo wa
kompyuta ulifanyika na kubaini kompyuta ilikuwa sahihi,”alisema.
Amesema makosa yaliyojitokeza katika karatasi zilizosahihishwa
kwa mkono ni kuweka pata pale ambapo kuna kosa ama kuweka
kosa pale ambapo kuna pata, makosa ambayo kwenye usahihishaji
wa kutumia kompyuta hakuwepo.
 
Matokeo ya dalasa la saba yaliyopachikwa hapo juu pia
yanapatikana katika tovuti za:
 
1.     www.necta.go.tz
2.     www.edu.udsm.ac.tz
4.     www.moe.go.tz 0 comments:

Post a Comment