ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A LOWEST COST AND ALSO SEND TO US NEWS, EVENTS FOR MORE INFORMATION CONTACT US TELEPHONE: +919160901191 E-mail: ally.shaaban@yahoo.com | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU NA PIA TUTUMIE HABARI, MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +919160901191 Barua Pepe: ally.shaaban@yahoo.com | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI HAPA

Thursday, February 16, 2012

SEMINA LA WATEULE WA KILI MUSIC AWARDS 2012 YAFANYIKA LEO JIJINI DAR

 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumwa wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wanamuziki walioingia kwenye kinyang'anyiro cha Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012 inayofanyika kwenye ukumbi wa JB Belmont,Benjamini Mkapa Tower,jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Tuzo za BASATA,Angelo Luhala akifafanua jambo kwa wanamuziki walioingia kwenye kinyang'anyiro cha Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012 wakati wa semina ya siku moja inayofanyika kwenye ukumbi wa JB Belmont,Benjamini Mkapa Tower,jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati Elekezi ya Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards,Innocent Nganyagwa a.k.a Ras Inno akitoa maelekezo ya Tuzo hizo kwa wanamuziki walioingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012 wakati wa semina ya siku moja inayofanyika kwenye ukumbi wa JB Belmont,Benjamini Mkapa Tower,jijini Dar es Salaam.

MASHINDANO YA KUTAFUTA TIMU YA TAIFA YA MASUMBWI YAENDELEA

Bondia Fabian Gaudence (kushoto) akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na Idd Pialali wakati wa mashindano ya kuchagua mabondia watakaowakilisha taifa katika mashindano ya Kimataifa yanayotaraji kufanyika hivi karibuni. Gaudence alishinda kwa pointi.
Mabondia Peter Stanley (kushoto) akipambana na Doto Shoka wakati wa mashindano ya kutafuta mabondia watakaoliwakilisha taifa katika mashindano ya Kimataifa. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete Akutana Naibu Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw.Erastus Mwencha,Naibu Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.Katikati ni Kamishna wa Maendeleo ya vijijini na Kilimo wa Kamisheni hiyo, Bi Rhoda Tumusiime waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo January 16, 2012. Viongozi hawa wako nchini kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Kilimo toka nchi Saba za Afrika unaofunguliwa kesho (January 17, 2012) Kilimanjaro Hyatt hotel jijini Dar es salaam.
Picha Na IKULU.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani laTaifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako Azungumza Juu Ya Kufutwa Kwa Mitihani Kwa Baadi Ya Skuli Zanzibar

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar matokeo ya kufutwa kwa mitihani kwa baadi ya Skuli kutokana na kufanya udanganyifu.mkutano huo umefanyika Hoteli ya Bwawani Zanzibar. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako, akionesha ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Uchunguzi ya Vyombo vya Usalama kuhusi undanganyifu wa baadi ya miandiko iliotumika katika mitihani ya watahiniwa wa Kidatu cha Nne.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Matihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichoka, akionesho karatasi za mitihani ambozo zimekuwa na miandiko zaidi ya mmoja na kufanana maneno ya majawabu.

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI ABAKA MTOTO WA MIAKA 13,ATOA HONGO KIASI CHA LAKI MBILI ILI KESI ISIENDE MBELE

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mwalimu wa shule ya msingi Bwato wilaya ya Kyela mkoani mbeya Bwana Herny Hans Mwaikokoba anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, mwenye umri wa miaka 13.
Tukio hilo likiwa ni la pili kwa mwalimu huyo kumtendea mtoto huyo, ambalo limethibitishwa na mtoto mwenyewe na shangazi yake aitwaye Bi Sabina Ndobo mkazi wa kijiji cha Bwato wilayani humo.
Mara ya kwanza mnamo Oktoba mwaka uliopita, mwalimu huyo alimtendea tukio hilo la kumbaka mtoto huyo na kisha kumpa shilingi 200, ili anunue mihogo na tukio la pili alilifanya Novemba mwaka uliopita ambapo alimpa shilingi 500, baada ya mtoto huyo kupiga kelele na kijana aliyekuwa akikaanga mihogo Bwana Mwarabu alimuokoa mtoto huyo.
Wakati mwalimu huyo akitenda kosa hilo alimtishia kumfukuza shule au kumuua mtoto huyo endapo atatoa siri hiyo.

WANUSURIKA KATIKA AJALI YA BASI MBEYA

Basi la Happy Nation limeanguka baada ya kushindwa kuumudu mteremko wa TAZAMA, maarufu kama Pipeline. Habari toka kwa abiria waliopanda basi la Nganga, anasema watu wamejeruhiwa vibaya ila hakuna vifo. Basi hilo likiwa kwenye mwendo kasi lilitaka kulipita basi la Nganga, lakini kukawa na gari jingine linapandisha mlima huo, ndipo dereva akalazimika kulirudisha nyuma ya basi la Nganga na kuligonga kwa nyuma na kupinduka. Abiria wa basi la Nganga wamesalimika wote.
Picha na Felix Mwakyembe.

MKAZI WA SINGIDA AHUKUMIWA KUPELEKWA TAASISI YA MAGONJWA YA AKILI KWA KIPINDI CHOTE CHA MAISHA YAKE KWA KOSA LA MAUAJI.

Jaji Mwanahamisi Kwariko.
====
Nathanel Limu.
Mahakama kuu kanda ya Dodoma inayoendelea na vikao vyake mjini Singida imemwamuru mshitakiwa Simon Andrew mkazi wa kijiji cha Kidaru wilayani Iramba, kupelekwa kwenye taasisi inayojishughulisha na magonjwa ya akili kwa kipindi chote cha maisha yake yaliyobakia hapa duniani.
Akitoa amri hiyo, Jaji Mwanahamisi Kwariko amesema mahakama yake imekubaliana na upande wa mashitaka kwamba mshitakiwa Simon alimuua bibi kizee Tiale Mbogo kwa kukusudia.

SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LAZINDUA KAMPENI YA KUPAMBANA NA UTAPIAMLO KWA WATOTO

 
Baadhi ya Wanafunzi hao wakiwa na Mh. Hilda Ngowi.
 Mh. Mbunge wa Viti Maalum toka mkoa wa Iringa Lediana Ng'ong'o akizungumza na waandishi wa habari ambapo ametoa ushauri kwa  serikali kuwaajiri wataalam wa lishe kwa kila wilaya ili kufanikisha malengo ya Mkakati wa Kitaifa wa Lishe wa 2011/12 hadi 2015/16.

 Mwanaharakati wa Haki za Watoto na Afya zao Bi. Hoyce Temu akizungumza na wanahabari kuhusiana na kampeni ya kupambana na utapiamlo kwa watoto, ambapo amesema tatizo hilo ni kubwa sana hapa nchini na kuishauri serikali ielimisha jamii umuhimu wa kula chakula bora na pia kutoa ufafanuzi kuwa chakula bora ni kipi.

JAMAA MWIZI WA SAA YA ROLEX AKAMATWA............KAMERA!!

Lauderdale Rolex Thief Caught On Camera
A passenger sends her $6,500 watch through the scanner but accidentally she leaves the watch in security bin .

Wednesday, February 15, 2012

WADAU MSAADA UNAHITAJIKA WA SHILINGI MILIONI 45 BEATRICE ATIBIWE INDIA!!

Baetrice Emanuel Kantimbo(48)

CCM IRINGA KUFUKA MOSHI ,WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM WATOFAUTIANA JUU YA KATIBU


Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bi.Mary Tesha
******
Wakati kesho chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kinakusudia kufanya mkutano wake wa Halmashauri kuu ya mkoa ,wajumbe wa mkutano huo wameonyesha kutofautiana na katibu wa CCM mkoa Bi.Mary Tesha na kupanga kutumia mkutano huo kumweka kitimoto ama kumkataa .
Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umedokezwa kuwa moja kati ya vikwazo vya CCM kuendelea kukataliwa na wananchi mkoani hapo ni kutokana na katibu huyo kufanya kazi kivyake vyake na kutowajali watendaji wengine.
Wadai kuwa hata wafanyabiashara na wadau mbali mbali waliokuwa wakichangia chama kwa sasa toka afike katibu huyo wameanza kurudi nyuma na kuwa zipo dalili za CCM mkoa wa Iringa kushindwa vibaya katika chaguzi kutokana na katibu huyo kujijali yeye zaidi kuliko chama na kuomba CCM Taifa kujaribu kufuatilia utendaji kazi wa katibu huyo wa mkoa ambaye wamemfananisha na mfanyabiashara
Na Francis Godwin.
BOFYA

NGOJA NIUDANGANYE MOYO!!

Airtel yaja na “Nani Mkali” promosheni

• Mamia kushinda fedha taslim
• Zaidi ya milioni 200 kuzawadiwa
15, Februari 2012 Siku moja baada ya Valentine Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imezindua promosheni mpya itakayowawezesha wateja wake kujishindia mamilioni ya fedha taslimu ijulikanayo kama “Nani
Mkali”
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (pichani kati) alisema “ leo Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania kushiriki na kushindafedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi. Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, kila siku kutakua na mshindi wa milioni moja,kila wiki milioni tatu na kila mwezi milioni thelathini(30).
Kuhusu jinsi ya kujiunga na “Nani Mkali”, afisa bidhaa wa Airtel bi Alice Paulsen alisema,”tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru katika promosheni hii mteja anatakiwa kuandika neno
“Mkali” na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa ili kujiunga. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu
utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.
Promosheni hii pia itatoa fursa kwa wateja kuchagua lugha wanayotaka kwa kutuma neno “swa” kwa Kiswahili au “eng” kwa lugha ya kiingereza kwenda namba 15595 Kujua alama ulizonazo au point mteja wetu atatakia kutuma neno “point” au “alama” kupatiwa pointi alizojikusanyia. Kujiondoa mteja atatakiwa kutuma neno “cancel’ au “stop” kujindoa kwenye promosheni.
Akitoa ufafanuzi zaidi Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando aliongeza kwa kusema promosheni ya “Nani Mkali” inazinduliwa leo ikiwa bado promosheni yetu kubwa ya Mzuka wa Airtel inaendelea ambapo wateja wanajishindi simu,muda wa maongezi pamoja na pesa taslimu zaidi ya
shilingi milioni 50.

KIFO CHA WHITNEY HOUSTON BOBY BROWN AHUSISHWA

Whitney Houston.

Bobby Brown.
******
Sifael Paul na Mtandao
KIFO cha staa wa muziki wa Pop, RnB na muvi za Hollywood, Marekani, Whitney Houston (48), kimeibua gumzo kubwa katika ulimwengu wa burudani, huku aliyekuwa mumewe kati ya mwaka 1992 hadi 2007, Boby Brown akihusishwa.
Kwa mujibu wa msemaji wa Whitney, Kristen Foster, Whitney alifariki dunia Jumamosi iliyopita katika Hoteli ya Beverly Hilton jijini Los Angeles, saa chache kabla ya ‘kupafomu’ kwenye sherehe za maandalizi ya Tuzo za Grammy, bado uchunguzi wa kifo chake unaendelea.

MWEKEZAJI KAPUNGA MBARALI MBEYA AFIKISHWA MAHAKAMANI

SERIKALI imemfikisha mahakamani Mwekezaji wa shamba la Mpunga la Kapunga lililopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya kampuni ya Expotr Trading Group amefikishwa mahakama ya wilaya ya Mbeya kwa makosa mawili tofauti likiwemo kosa la kula njama la kutenda kosa la kuharibu mali na kuharibu mali za wananchi kwa hila.
Mwekezaji huyo alifikishwa mahakamani hapo jana kwa makosa hayo aliyoyatenda Januari 12 hadi 14, mwaka huu kwa kutumia ndege ya kunyunyizia dawa ambapo alimwaga sumu katika mashamba ya wakulima zaidi ya 154 wa Kijiji cha Kapunga wilayani humo.
Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Seif Kulita, Mwendesha mashitaka wa Serikali Griffin Mwakapeje alisema kuwa washitakiwa hao aiwemo Meneja wa shamba hilo Walder Vermaak, Afisa ugani Serger Bekker na Rubani wa ndege Andries Daffe walitenda kosa hilo wilayani humo na kuharibu mazao ya wakulima hekari 489.5.
Mwakapeje alisema kuwa wawekezaji hao wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na sheria namba 226 (i) cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2002 la kuharibu mazao hayo ya Mpunga wa wakulima wanaolima eneo linalojulikana kwa jina la Mpunga moja.
Baada ya mashitaka hayo, Hakimu Kulita alpowauliza washitakiwa hao wote kwa pamoja walikana shitaka hilo ambapo wakili anaowatetea watuhumiwa hao Ladislaus Rwekaza aliomba dhamana kwa wateja wake na hatimaye mahakama ikaridhia kwa Masharti ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja mweye mali isiyohamishika isiyopungua Shilingi Milioni kumi.
Aidha Hakimu huyo alitoa sharti kwa watumumiwa hao kuwa mbali na sharti la kuwa na mdhamini mmoja na mali isiyohamishika pia watuhumiwa waliytakiwa kukabidhi hati za kusafiria na kwamba hawapaswi kusafiri nje ya mkoa wa Mbeya na kama watahitaji kusafiri nje ya mkoa wa Mbeya ni lazma wapate kibali cha mahakama hiyo ambapo washitakiwa walitimiza masharti hayo.
Baada ya Masharti hayo watuhumiwa walidhaminiwa na Uwesu Msumi mkazi wa Jijini Dar Es Salaam na kukabidhi hati ya nyumba yenye namba 229 Block J iliyopo Mbezi Jijini Dar es Salaam, Christian Basil Mmas aliyekabidhi hati ya nyumba yenye namba 109 iliyopo Geza Ulole Jijini Dar es Salaam na Sunnil aliyetoa hati namba 254 iliyopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam na kesi hiyo itatajwa tena Machi 6, mwaka huu.
Baadhi ya wananchi walioathiriwa na sumu hiyo wakati ndege ikimwaga mashambani na kushuhudiwa ni pamoja na Michael Shija, Severina Mbwilo, Elikana Nsemwa, Edward Simkoko, Gaidon Peter Ngogo (54), Jailo Esau (22), Jackson Mwandemange (52), Catherina Shipela (50), Edda Ngosha (35), Julius Isega(50), Ramadhan Nyoni (52)
CHANZO: BOFYA
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUSOMA HABARI ZILIZOPITA BOFYA NENO OLDER POSTS HAPO JUU ASANTE SANA KWA KUTEMBELEA NA KARIBU TENA