Mratibu wa mradi wa Shuga akijibu maswali yaliyokua yanaulizwa na kikundi cha wasikilizaji cha Iwawa- Makete mkoani Njombe.
Wakionyesha furaha zao baada ya kuelewa mada ya siku ukihusianisha na maisha yao ya kila siku
Mwezeshaji
wa kikundi cha wasikilizaji wa Kihesa, Manispaa ya Iringa mjini
akitimiza jukumu lake la kuelimisha wenzake na kuwawezesha kushiriki
katika majadiliano baada ya kusikiliza kipindi |
Vijana
wa Iringa wakionyesha nyuso zenye furaha baada ya kuongeza uelewa
kupitia majadiliano baada ya kipindi cha saba cha mfululizo wa vipindi
vya Shuga
|
Kikundi
cha wasikilizaji kutoka kijiji cha Kabanga, Kyela wakifurahia uelewa
walioupata juu ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba katika maisha
yao
|
Kikundi cha wasikilizaji Jitambue 1 kutoka wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wakijadiliana sehemu ya saba ya mfululizo wa vipindi vya mchezo wa redio wa Shuga. |
Wakina mama wakifuatilia mjadala kuhusu kujitambua na namna ya kujikinga na Virusi vya UKIMWI pamoja
|
Mwana kikundi wa AMKA- Njombe vijijini akiwashirikisha wanakikundi wenzie uzoefu wake katika kukabiliana na changamoto za kutakwa kimapenzi na wanaume waliomzidi umri |
Mwanachama
ambaye amekua baba katika umri wa miaka 19 akionyesha shukrani zake kwa
vipindi vya Shuga kwa kumuwezesha kujitambua, kwenda kupima afya yake
na kujiwekea malengo ya kujilinda yeye, mama pamoja na mtoto dhidi ya
maambukizi ya VVU
|
Tunajitambua, Tunajipenda na Tunajilinda na VVU. Tumepima - Kikundi cha AMKA kutoka Njombe
|
UGONJWA
wa UKIMWI umekuwa janga kubwa sana duniani huku wadau mbalimbali
wakiendelea kutoa elimu na kuhamasisha katika kuanzisha programu
mbalimbali za kubadilisha tabia chanya kwa jamii.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki, Mratibu wa mchezo wa redio wa Shuga alisema tayari
wameanzisha programu mbalimbali za vipindi vinavyolenga kuelimisha jamii
hususani vijana juu ya maambukizi ya Virusi vya ukosefu wa kinga
mwilini (UKIMWI), usawa wa jinsia, kufanya maamuzi sahihi, matumizi
sahihi ya kinga na kuepukana na msongo rika.
Alisema mfululizo huu wa mchezo wa redio wa Shuga unawalenga zaidi
vijana hususan wasichana, kwa kuangalia mtazamo wao, matarajio pamoja
na changamoto wanazopitia kwa njia sahihi za kukabiliana na changamoto
ili kutimiza malengo yao.
"Mchezo wa redio wa Shuga ulianzishwa mnamo mwaka 2014 kwa ushirikiano
kati ya MTV, HIV and AIDS Free Generation, Shirika la TACAIDS pamoja na
UNICEF. Baada ya mafanikio makubwa msimu wa kwanza, TACAIDS na UNICEF
pamoja na wadau wengine waliamua kupanua wigo wa program hii kwa kuandaa
vipindi zaidi ili kuimarisha tabia chanya zilizojengwa katika msimu wa
kwanza wa vipindi vya Shuga," alisema Laizer
Alisema mfululizo wa vipindi vya redio vya Shuga awamu ya pili vilianza
kupitia redio mbalimbali nchini kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa nne
2016 kwa lengo la kuendeleza elimu ya masula ya UKIMWI.
"Katika kuboresha utoaji elimu kuhusiana na maudhui ya vipindi, kampuni
ya True Vision Production imefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa awamu
ya pili ya mfululizo wa vipindi vya redio vya Shuga katika kuhakikisha
jamii inakuwa na uelewa juu ya masuala hayo." alisema Laizer. "Kwa sasa,
vituo mbalimbali vya redio vinarusha sehemu ya nane ya mfululizo wa
vipindi vya Shuga." Aliongezea Laizer.
Alisema
Matokeo ya mradi huu yameanza kuonekana na vijana ambao ni walengwa
wakuu wametoa ushuhuda wao kuhusiana na kipindi hicho cha Shuga na
kusema kuwa klipindi kimewaletea mabadiliko makubwa.
‘Vijana
tunajitambua, tumehamasika kwenda kupima afya zetu, tunajua njia sahihi
za kujilinda na magonjwa ya zinaa na pia tunajiwekea mipango endelevu,"
alisema Abbas Boniphace, mmoja wa wasikilizaji wa kipindi cha Shuga
kutoka Njombe
"Ningepata
nafasi ya kusikia Shuga mapema nisingepata ujauzito katika umri mdogo.
Sikua na uelewa wakati huo, sasa najitambua, nimepima na najilinda,
siwezi kudanganyika" alisema Herieth kutoka Njombe.
"Wazazi
huogopa kutuambia ukweli juu ya maswala yahusuyo VVU na UKIMWI ila
Shuga inaelezea kwa uwazi zaidi." Alisema Shamila Juma, mwana kikundi cha wasikilizaji wa vipindi vya Shuga
0 comments:
Post a Comment