Azam, Coastal kuzindua U-20
Basi la timu ya Azam
Na Vicky Kimaro, Mwananchi
Michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu inaanza kutimua vumbi Novemba 17, kwenye Viwanja vya Karume na Azam Complex, Dar es Salaam.
•Ratiba ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Maji Uhai imefanyika jana mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo timu zimepangwa katika makundi matatu
Michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu inaanza kutimua vumbi Novemba 17, kwenye Viwanja vya Karume na Azam Complex, Dar es Salaam.
•Ratiba ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Maji Uhai imefanyika jana mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo timu zimepangwa katika makundi matatu
Kundi A linaundwa na mabingwa watetezi Azam, Coastal Union, JKT Ruvu, Mbeya City na Yanga, wakati Kundi B ni Ashanti United, Mgambo Shooting, Oljoro JKT na Ruvu Shooting. Huku Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Rhino Rangers na Tanzania Prisons zipo Kundi C.
Mechi za ufunguzi Kundi A kati ya Azam na Coastal Union (saa 2 asubuhi- Karume), Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana- Karume). Kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi- Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni- Karume).
Kagera Sugar na Mtibwa Sugar (saa 2 asubuhi- Azam) na Rhino Rangers na Tanzania Prisons (saa 10 jioni- Azam) ndizo zitakazocheza mechi za ufunguzi Novemba 17 mwaka huu katika kundi C.
Robo fainali ya michuano hiyo itachezwa Novemba 24 na 25, wakati nusu fainali itapigwa Novemba 26 na 27. Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na ile ya fainali zitachezwa Novemba 30 mwaka.
Azam anatetea ubingwa huo baada ya kuinyuka Coast Union msimu uliopita katika fainali na kufanikiwa kutwaa Sh 1.5 milioni huku Coast wakiwa washindi wa pili walipata Sh1 milioni na Simba ikaambulia Sh500,000 baada ya kuibuka mshindi wa tatu baada ya kuinyuka Mtibwa Sugar.
Michuano hii imekuwa chimbuko la wachezaji wengi chipukizi wanaotamba kwa sasa katika Ligi Kuu.
CHANZO: MWANANCHI
LEWANDOWSKI AITEKETEZA ARSENAL, CHELSEA YAUA LIGI YA MABINGWA, BARCA NA AC MILAN 1-1
BAO la dakika za lala salama la Robert Lewandowski limeipa ushindi wa 2-1 Borussia Dortmund dhidi ya Arsenal katika Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Emirates usiku huu.
Henrikh Mkhitaryan aliifungia bao la kuongoza Borussia Dortmund, lakini Olivier Giroud akasawazisha ikawa 1-1.
Lakini katika dakika 10 za mwisho, Arsenal ikatepeta na kumruhusu mshambuliaji Lewandowski kuwamaliza nyumbani.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Arteta, Wilshere, Ozil, Rosicky na Giroud.
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Grosskreutz, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender, Sahin, Blaszczykowski, Mkhitaryan, Reus na Lewandowski.
Katika mchezo mwingine, Chelsea imeshinda ugenini mabao 3-0 dhidi ya Schalke yaUjerumani, mabao ya Fernando Torres mawili na Eden Hazard moja.
Nayo AC Milan imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Barcelona katika mechi ya Ligi ya Mabingwa usiku huu Uwanja wa San Siro.
Robinho alitangulia kuwafungia wenyeji bao dakika ya tisa, pasi ya Mbrazil mwenzake, Kaka- lakini Lionel Messi akaisawazishia Barca dakika ya 24 kwa pasi ya Iniesta.
Mechi nyingine, Steaua Bucuresti imetoka 1 - 1 na
Basel, Olympique Marseille imefungwa 2-1 na Napoli, Porto imelala 1-0 mbele ya Zenit, Austria Wien imefungwa 3-0 na Atletico Madrid na Celtic imeshinda 2 - 1 dhidi ya Ajax.
Mechi nyingine, Steaua Bucuresti imetoka 1 - 1 na
Basel, Olympique Marseille imefungwa 2-1 na Napoli, Porto imelala 1-0 mbele ya Zenit, Austria Wien imefungwa 3-0 na Atletico Madrid na Celtic imeshinda 2 - 1 dhidi ya Ajax.
==================================================================
Mechi ya Wahariri na Klabu ya Waandishi Iringa sasa rasmi
Nahodha wa timu ya soka ya Wahariri nchini Kulwa Karedia akiongea na waandihsi wa habari(hawapo pichani)muda mfupi kabla ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya timu yake na ya wanahabari wa mkoa wa Iringa vyenye thamani ya Sh 3 Milioni. Timu mbili hizo zinakutana kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa mjini Iringa mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akikabidhi kwa Nahodha wa Timu ya Soka ya Wahariri Kulwa Karedia vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya timu yake na ya wanahabari wa mkoa wa Iringa vyenye thamani ya Sh 3 Milioni. Timu mbili hizo zinakutana kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa mjini Iringa mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wa kwanza kushoto) na Nahodha Msaidizi Saleh Mohammed
Kutoka Kulia Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Nahodha Msaidizi wa Timu ya Soka ya Wahariri Saleh Mohamed, Nahodha wa timu hiyo Kulwa Karedia na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wakionesha sehemu ya vifaa mbalimbali vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kuwezesha mechi kati ya timu ya Wahariri na Timu ya wanahabari wa Mkoa wa Iringa. Mechi hiyo itachezwa mwishoni mwa wiki mjini Iringa.(P.T)
Mechi ya Wahariri na Klabu ya Waandishi Iringa sasa rasmi
Timu ya soka ya Jukwaa la Wahariri Nchini – TEF na ile ya Wanahabari wa Mkoa wa Iringa leo zimepokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki utakaochezwa mwishoni mwa wiki mjini Iringa.
Vifaa vilivyokabidhiwa leo na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim kwa Nahodha wa timu ya Wahariri ambae pia ni Mhariri Mkuu wa Habari wa Gazeti la Mtanzania Kulwa Karedia ni pamoja na jezi seti tatu, viatu, mipira, suti za michezo na soksi.
Akikabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es salaam, Mwalim amesema ni matokeo ya Vodacom kutambua umuhimu wa michezo na namna ambavyo Wahariri wanavyohitaji muda wa kushiriki michezo kwa afya na burudani kutokana na uasili wa majukumu yao ya kila siku.
"Tunafahamu jinsi kazi za Wahariri zilivyo hivyo hii ni fursa nzuri kwao kufanya jambo tofauti ili waweze kuwa na Wakati wa kuburudisha akili nje ya maeneo yao ya kazi tunaamini ni tukio zuri na muhimu kwao"Alisema Mwalim
"Wanahabari wamekuwa wadau wetu wakuu katika biashara hasa pale tunapohitaji kuupasha umma juu ya shughuli zetu mbalimbali hivyo nasi leo tunajisikia furaha kuwezesha tukio lao." Aliongeza
Mwalim amesema Vodacom inatambua umuhimu wa michezo na ndio maana imekuwa mdau mkubwa wa kuchangia maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini kwenye ngazi mbalimbali kuanzia ligi kuu hadi michezo ya ngazi za chini..
Kwa upande wake Karedia ameishukuru kampuni hiyo kwa kuiwezesha mechi hiyo jambo ambalo linaonesha jinsi kampuni hiyo ilivyo karibu na wanahabari nchini.
"Tunategemea kupata ushindani mkubwa kutoka kwa wanahabari wa mkoa wa Iringa nasi katika kuhakikisha tunatimzia azima ya ushindi timu yangu imekuwa kwenye mazoezi na tunaahidi kubeba zawadi ya ushindi."Aliongeza
"Tunayofuraha kubwa sana kuona Vodacom ikituunga mkono kutuwezesha mechi yetu ikifana,vifaa hivi tunavipokea kwa furaha na tunaahidi kurudi na ushindi."Alisema Karedia
Amesema maandalizi ya mechi hiyo yamekamalika na kwamba itafunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.Christine Ishengoma
Mbali ya kuzipatia vifaa timu zote mbili, Vodacom imetoa pia seti moja ya jezi na mipira minne kwa ajili ya zawadi ya mshindi wa mechi hiyo.
Mbali ya kuidhamini mechi hiyo, Kampuni ya Vodacom imechangia pia Shilingi 12 Milioni kwenye maandalizi ya Mkutano Mkuu huo wa TEF uliopangwa kufanyika kwa siku mbili Oktoba 25 na 26 Mjini Iringa.
Mwisho.
*****========******
MAN UNITED YAUA 4-2 ULAYA, ROONEY APIGA 2
Wayne Rooney Akifunga bao (HM)
Hadi sasa, Moyes wakati wote amekuwa akijaribu kuwatumia pamoja Robin van Persie na Wayne Rooney pale mbele. Sasa wako upande wake na wanamfanyia kazi nzuri.
Van Persie amefunga moja ya mabao ya msimu, Rooney amefunga mawili na lingine Antonio Valencia katika ushindi ho na sasa wanaelekea kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao, Manchester City wakiwa wenye kujiamini.
Faraja kwa Rooney leo ametimiza mabao 200 ya kuifungia United, hivyo kuingia kwenye orodha ya magwiji wa klabu, Bobby Chartlon mabao 249, Dennis Law 237 na Jack Rowley 211.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Damir Skomina wa Slovenia, Rooney alifunga dakika ya 22 na Bayer wakasawazisha kupitia kwa Rolfes dakika ya 54, kabla ya Van Persie kufunga la pili dakika ya 59, Rooney tena la tatu dakika ya 70 na Valencia dakika ya 79 kabka ya wageni kupata bao la pili dakika ya 88 kupitia kwa Toprak.
Kikosi cha Man Utd kilikuwa: De Gea, Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia, Carrick, Fellaini/Cleverley dk81, Kagawa/Young dk71, Rooney/Hernandez dk84 na Van Persie.
Bayer Leverkusen: Leno, Donati, Spahic, Toprak, Boenisch, Can, Reinartz, Rolfes, Sam/Kruse dk78, Kiessling/Derdiyok dk78 na Son/Benderdk 64.Uteuzi wa timu wa Moyes unamaanisha Ryan Giggs atasubiri sana kuongeza idadi ya mabao yake.
Mkongwe huyo wa United, akiwa amebakiza miezi miwili kusherehekea kutimiza miaka 40, amefungana kwa na gwiji wa zamani wa Real Madrid, Raul katika kucheza mechi nyingi katika Ligi ya Mabingwa, wote 144).
Na kwa kuwa Giggs hakuwepo hata benchi, kuna uwezaekano ikamchukua muda sana. Giggs na Raul wanafuatiwa na Paolo Maldini (mechi 140), Xavi (mechi 136), Clarence Seedorf (mechi 131), Paul Scholes (mechi 130) na Iker Casillas (mechi 129).
Chanzo:
binzubeiry
==============================================
VAN PERSIE ATAKA KUONGEZA MKATABA MAN U
Van Persie (HM)
Van Persie alikuwa na mwanzo mzuri katika msimu wake wa kwanza Old Trafford, akitwaa kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu England kwa mara ya pili mfululizo na kuiwezesha United kutwaa taji Barclays.
Inamaanisha Mholanzi huyo hakukosea kuondoka Arsenal na kuhamia kwa wapinzani wao wao.
Akizungumza na mshindi wa zamani wa Kombe la Ulaya na United, Paddy Crerand katika mahojiano maalum ya Televisheni ya klabu hiyo, MUTV, Van Persie alisema anataka kuendelea kuichezea zaidi klabu hiyo.
"Nina mika mitatu zaidi mbele, ningependa kukaa zaidi,"alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. "Nafahamu, na ninaona watu walionizunguka, kufanya maamuzi ambayo nafikiri hao watu wanaweza kugeuka na kusema; "Yalikuwa ni mazuri?". Sitaki hivyo.
"Nataka kucheza muda mrefu kadiri inavyowezekana katika kiwango cha juu,".
Kushinda mataji ndio kitu kinachomvutia zaidi Van Persie, ambaye hakuwahi kushinda chochote akiwa Arsenal tangu walipotwaa Kombe la FA kwa kuifunga United kwenye Fainali mwaka 2005.
Chanzo: binzubeiry
SHINDANO LA KUTAFUTA WIMBO WA YANGA KUPITIA RADIO CLOUDS FM
Dawati la habari za michezo na burudani Clouds Fm.
Mmoja kati ya watangazji maarufu wa radio Clouds Fm Bw Ephraim kibonde
Uongozi wa Mabingwa wa Soka nchini Yanga ya jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Clouds Media kupitia radio yake ya Clouds kwa pamoja wamezindua shindano la kutafuta wimbo maalumu wa Klabu ya Yanga utakaoshindaniwa na Wasanii mbalimbali hapa nchini ambao wimbo huo utakapopatikana utatumika katika mashindano mbalimbali pamoja na shughuli za klabu hiyo.
Taarifa hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam hii leo na Ally Mayayi ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Klabu ya Yanga ambaye pia ni mjumbe wa Kamati inayosimamia zoezi zima la upatikanaji wa wimbo maalum wa Klabu hiyo.
Mayayi amesema uzinduzi huo umefanyika Januari 29 Mwaka huu jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kukamilika Februari 7 Mwaka huu.Katika kufanikisha zoezi hilo linafanikiwa jumla ya nyimbo kumi bora zitachaguliwa na wanachama wa Klabu hiyo kwa aajili ya kupata wimbo mmoja ambao utakuwa ni mahususi utakaotumika katika mambo mbalimbali ikiwemo michuano ya ndani nchi pamoja na ya kimataifa ikiwemo shughuli za Kimaendeleo za Klabu ya Yanga. alisema Mayayi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo mara baada ya kupatikana kwa wimbo huo maalum Msanii na wimbo huo utatangazwa katika sherehe za Yanga Day zinazotarajiwa kufanyika Februari 12 Mwaka huu jijini Dar es Salaam na mshindi aliyepatikana anatarajiwa kukabidhiwa zawadi yake.
Klabu ya Yanga moja ya Klabu Kongwe hapa nchini hivi karibuni ilianzisha Kampeni ya kutafuta wimbo maalum kama kitambulisho kwa wapenzi na wanachama wa Klabu hiyo. Wimbo pekee ambao ulikuwa ukitumika katika shughuli mbalimbali zinazohusu klabu ya Yanga ni ule uliotungwa na Mwanamuziki Pepe Kalle Yanga Africa Mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati ambao unatumika katika vituo mbalimbali vya radio hapa nchini.
Afisa Habari - Young Africans Sports Club ( YANGA)
**********************
TENGA ACHAGULIWA TENA CECAFA
Leodgar Tenga.
Taifa Stars yarejea nyumbani baada ya kuadhibu Chad 2-1
Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars Jan Paulsen akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo, mara baada ya timu hiyo kuwasili ikitokea N'Djamena nchini Chad, ambako ilicheza na timu ya taifa ya nchi hiyo na kuifunga magoli 2 kwa 0. Timu hizo zitarudiana siku ya jumanne wiki hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Taifa Stars inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kuingia katika hatua ya makundi kwa ajili ya kinyang'anyiro cha kushiriki kombe la dunia mwaka 2014 nchini nchini Brazil.
Kulia ni Mchezaji wa Taifa Stars Nizar Khalfan na kushoto ni Henry Joseph wakiongoza wenzao wakati walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu J.K.Nyerere leo jijini Dar es laam wakitokea nchini Chad.
Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars Jan Paulsen akiingia kwenye basi la timu hiyo, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere DIA jijini Dar es salaam.
Golikipa watimu ya taifa Juma K. Juma akiwa katika pozi katika basi la Taifa Stars leo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers (SBL) Teddy Mapunda na Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo kushoto, wakiwapongeza wachezaji wa Taifa Stars, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo alasiri.
Mwandishi wa habari wa BBC nchini David Eric Nampesya akimhoji katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Angetile Osiah wakati wa mapokezi ya Taifa Stars iliyowasili nchini leo ikitokea nchini Chad.
Mwandishi wa habari wa BBC nchini David Eric Nampesya akipozi kwa picha na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers (SBL) Teddy Mapunda.
Mzungu huyu ambaye hakufahamika jina lake mara moja, akipata taswira baada ya kuvutiwa na vijana hawa wanaofanya kazi ya promosheni ya bia ya Serengeti Lager.
Wachezaji hawa wa kesho nao wameshiriki kuwapokea kaka zao Taifa Stars wakati walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo.
Mashabiki mbalimbali wamejitokeza kuja kuwapokea wachezaji wa timu yao Taifa Stars ilipowasili leo ikitokea nchini Chad.