Wapiganaji wameshambulia kwa
risasi msafara wa vikosi vya kujihami vya nchi za magharibi NATO karibu
na mji mkuu wa Pakistan,Islamabad.
Waliwaua watu saba na kuchoma moto magari
kadhaa kabla ya kutoroka. Polisi wamesema kuwa zaidi ya watu 12
walihusika wakiwa wamejihami kwa magruneti na vilipuzi vingine.
Shambulio hilo lilitokea 10KM kutoka mji huo wa Islamabad.
Mwandishi wa BBC mjini humo amesema kuwa hii ni
mara ya kwanza kwa shambulio kama hilo kutokea karibu sana na mji mkuu.
Magari hayo ya NATO yalikuwa yanasafirisha
bidhaa kwa wanajeshi wao nchini Afghansitan.
BBC SWAHILI
BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment