SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, June 9, 2010

Mawaziri kushitakiwa kwa ufisadi, Uganda


Bendera ya Uganda
Mwendesha mashtaka mwandamizi nchini Uganda amethibitisha kuwa atawafungulia mashtaka ya ufisadi makamu wa rais wa nchi hiyo pamoja na waziri wa mambo ya nje.
Makamu wa rais Gilbert Bukenya, na waziri Sam Kutesa ni miongoni mwa viongozi wa serikali wanaoshutumiwa kwa wizi wa zaidi ya $25M wakati wa mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Madola, Commonwealth mnamo mwaka wa 2007.

Nchi ya Uganda
Waandishi wamesema kuwa uchunguzi huo umekuwa ukiendelea kwa muda japo lazima kwanza idhini itoke bungeni kabla ya hatua yoyote ya kisheria kuchukuliwa dhidi ya washukiwa hao
          *******************
Mawaziri watatu wa Somalia wajiuzulu
Mawaziri watatu wa serikali ya mpito ya Somalia wamejiuzulu. Akizungumza mjini Mogadishu hapo jana, waziri wa ulinzi Mohammed Siad amesema kuwa anajiondoa kutoka serikalini kwa kuwa imeshindwa kuweka uongozi thabiti nchini humo.
Mawaziri wengine waliojiuzulu wakiwa London ni Mohammed Abdillahi wa elimu na Hassan Maalim wa ofisi ya rais.
Wadadisi wanasema kuwa hatua ya kujiuzulu kwa mawaziri hao inahujumu serikali hiyo ya mpito ambayo tayari imekumbwa na matatizo mengi.
Somalia
Zaidi ya thuluthi mbili ya Somalia inashikiliwa na wapiganaji wa kiislamu. Nchi hiyo haijawahi kupata serikali thabiti tangu 1991.
BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment