Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Askari
polisi watano mkoani dodoma wamefariki dunia papohapo katika ajali ya
gari iliyotokea 31/01/2014 majira ya saa 5 usiku katika barabara kuu ya
Dodoma – Morogoro eneo la Mtumba Center, Kata ya Mtumba Tarafa ya
Kikombo Manispaa ya Dodoma, ambapo gari namba ya usajili T.770 ABT
Toyota Corolla lililokuwa likiendeshwa na Askari mwenye namba H. 3783 PC
DEOGRATIUS wa Wilaya ya Kongwa.Gari hilo lilikuwa likitokea Dodoma
mjini likielekea Wilayani Kongwa liligongana uso kwa uso na gari namba
T.997AVW Scania Bus mali ya Kampuni ya Mohamed Trans lililokuwa
likiendeshwa na JUMA s/o MOHAMED, miaka 38, Mkazi wa Mwanza, likitokea
Dar es Salaam kuelekea Dodoma na kusababisha vifo kwa askari watano
papohapo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME amewataja Askari hao waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni:-
1. D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye miaka 51, Mgogo.
2. F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye miaka 34, Muha.
3. H.3783 PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
4. WP.10337 PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
5. WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye miaka 20, Mhehe.
Wote ni askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.
Kamanda
MISIME amesema chanzo cha ajali hiyo kulingana na uchunguzi wa awali ni
mwendo kasi kutokana na uharibifu uliotokea kwa gari dogo walilokuwa
wamepanda askari na jinsi lilivyoburuzwa na basi kwa umbali wa mita 56
kisha kwenda kusimama umbali wa mita 97, kwa hali hiyo umbali kutoka
eneo walipogongana hadi basi liliipoenda kusimama ni mita 152. Dereva wa
Bus alitoroka mara baada ya ajali hiyo kutokea, juhudi za kumtafuta
zinaendelea. Miili ya marehemu imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali
ya mkoa Dodoma.
Aidha
Kamanda MISIME ametoa wito kwa madereva kila mara wawe na udereva wa
tahadhari na na kuzingatia sheria za usalama barabarani.
KWA HISANI YA SOPHIEMBEYU BLOG
KWA HISANI YA SOPHIEMBEYU BLOG
0 comments:
Post a Comment