Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wa pili kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa kwanza kulia) wakiwa kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili nchini tangu novemba 2015 hadi novemba 2016, uliowakutanisha wadau wa Maliasili kutoka sekta binafsi na Serikalini kujadili sekta za misitu , wanyampori pamoja na mambo kale ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Eng. Angelina Madete akichangia hoja kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili nchini tangu novemba 2015 hadi novemba 2016.Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wa akiwa na wadau wa Maliasili wakisiliza kwa makini uwasilishaji wa mada kuhusu sekta za misitu , wanyampori pamoja na mambo kale kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili nchini tangu novemba 2015 hadi novemba 2016.
Baadhi ya wadau wa Maliasili kutoka serikalini na Sekta binafsi wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa mada za Maliasili kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili nchini tangu novemba 2015 hadi novemba 2016.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa hakuna magogo na malighafi ya misitu yatakayosafirishwa kwenda nje ya nchi kabla ya kuchakatwa.
Amesema , hiyo itasaidia kuongeza thamani pamoja na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wengi kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kutengezea vifaa mbalilmbali vitakanavyo na mazao ya misitu kutokana na Magogo na Malighafi ya misitu kuchakatwa ndani ya nchi.
Amesema hayo leo kwenye mkutano wa kutathmini mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili nchini tangu novemba 2015 hadi novemba 2016, uliowakutanisha wadau wa Maliasili kutoka sekta binafsi na Serikalini kujadili sekta za misitu , wanyampori pamoja na mambo kale
Amesema kuwa Misitu ni sekta inayokabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukataji miti hovyo uvunaji haramu wa magogo pamoja na usafirishaji haramu wa magogo kwenda nje ya nchi.
Amesema katika kukabiliana na changamoto hizo Serikali imeanza kuona namna ya kuwalipa sekta binafsi na watu wenye kipato cha chini cha kati watakaokuwa wanapanda miti kama motisha kutokana na mchango mkubwa wa misitu wa kuzalisha hewa safi duniani kwa kuondoa hewa ya ukaa.
Amesema mpango huo kamambe wa kuwalipa watakaopanda miti kwa wingi itakuwa ni njia muafaka ya kuondokana na tatizo la ukame linaaloendelea kutokea kutokana miti mingi kuendelea kukatwa kwa ajili ya mkaa na matumizi mengine kuongezeka kwa kasi.
0 comments:
Post a Comment