SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, April 29, 2012

Cheka ashinda gari jana kwa kumtwanga Maugo na kupata nalo ajali leo

 Cheka akivishwa mkanda wa ushindi wa IBF
 Meya wa Manspaa ya Ilala Jery Slaa akimkabidhi funguo ya gari bondia Francis Cheka baada ya kuibuka na ubingwa wa K.O raundi ya 6 jana
****
Jana usiku katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam kulifanyika mpambano wa kuwania ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka (Morogoro) na Mada Maugo (Dar es Salaam).
Pambano hilo lilikuwa la raundi 12 lakini ilipofika raundi ya sita kabla ya kuanza raundi ya saba, Maugo alitangaza kutokuendelea na mchezo kwa kile alichodai kuishiwa na pumzi na kusema, '...sirudi, jmaa ataniua...' huku akivua "gloves" na hivyo kumpa Cheka kwa Technical Knock Out "TKO", uamuzi ambao ulimpa Cheka mkanda wa Ubingwa wa IBF  pamoja na gari (pichani).
Furaha ya ushindi huo imegeuka huzuni leo baada ya Cheka kupata ajali ya gari alilokabidhiwa jana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, akizungumza na "SufianiMafoto"alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea jana usiku majira ya saa nane maeneo ya Manzese na kuwajeruhi dereva na abiria wake waliokuwa katika pikipiki hiyo. Alisema baada ya ajali, dereva wa gari hilo lenye namba za usajili T 321 AAU, aliyefahamika kwa jina la Francis Cheka, alifikishwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na kushikiliwa hadi asubuhi ya leo walipofika ndugu zake na kumwekea dhamana. 
Akielezea tukio hilo la ajali, Kenyela alisema kuwa gari la Cheka lilikuwa likitokea maeneo ya Manzese kuelekea Ubungo na pikipiki ilikuwa ikitokea Ubungo kuelekea Manzese na walipofika maeneo ya Tip Top Manzese, dereva wa pikipiki alihamia barabara ya pili ili kuelekea Ubungo na ndipo alipogongana na gari hilo. Aidha alisema kuwa dereva huyo wa pikipiki bado amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala akiendelea na matibabu huku abiria wake akitibiwa usiku wa jana na kuruhusiwa.  

0 comments:

Post a Comment