SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 2, 2012

MAHIZA AHIMIZA WAFANYAKAZI KUWA WAADILIFU

Mahiza akiwahutubia wakazi wa Dar es Salaam Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Sehemu ya umati uliofika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi.
Wakazi wa Dar es Salaam wakiwa na gazeti la Uwazi linalotolewa na kampuni ya Global Publishers kila Jumanne.
Bendi ya Jeshi la Magereza ikitoa burudani.
Kinamama wakifurahia Mei Mosi.
Watoto wa shule pia waliokuwepo kwa wingi.
Mmoja wa washindi wa zawadi ya Mfanyakazi Bora.
Kijana akionyesha sarakasi katika sherehe hizo.
Mama mlemavu akitafuta nafasi nzuri ya kufaidi sherehe hizo.
Viburidisho vilikuwepo kwa wingi.
Mkazi wa Dar akipumzisha akili katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi akiwa anapiga picha ya pamoja wa baadhi ya maofisa wa serikali na wale walioibuka kuwa wafanyakazi bora.
Mahiza akiondoka Mnazi Mmoja.
MKUU wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Mwantumu Mahiza, amewaasa wafanyakazi wa kila sekta nchini kufanya kazi  kwa bidii na uadilifu mkubwa.
Aliyasema hayo leo katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi iliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo  sherehe za kitaifa zimefanyika Mkoa wa Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani na mgeni rasmi akiwa Rais wa Muungano, Jakaya Kikwete.
HABARI/PICHA: HARUN SANCHAWA, GPL

0 comments:

Post a Comment