Mwanafunzi wa Madrasa AL-Mustakima Rashid Kimweli akisoma Quaran katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quaran yaliyofanyika mbagala bucha, jijini Dar es salaam wakati wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quran yaliandaliwa na Madrasa ya AL-Mustakima iliyopo Mbagala Bucha jijini Dar es salaam ambapo watoto wa kiislamu takribani 10 wenye umri kati ya miaka sita hadi 13 wa madrasa nne za Madrasa Tul – Mustakima ya Yombo Dovya, Mbagala Bucha, Madrassa Tul- ukutani na madrassa Tul Ismailia ya mtoni kijichi.
Mwanafunzi wa madrasa AL-Mustakima Zahra Mohamedi akipokea zawadi shilingi laki moja na thelathini na tano ( 135,000) kwa kuibuka mshindi wa kwanza wa kusoma na kuihifadhi juzuu tano kati ya thelathini katika kitabu cha Quaran.
Mwalimu mkuu wa Madrasa AL- Mustakima Ustaadhi Hassani Seleiman akimtunza fedha ustaadh Iddrisa wakati wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quran yaliyoandaliwa na Madrasa AL mustakima ya Mbagala bucha jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi wa madrasa AL-Mustakima akipokea zawadi shilingi laki moja na thelathini na tano ( 135,000) kwa kuibuka mshindi wa kwanza wa kusoma na kuihifadhi juzuu tano kati ya thelathini katika kitabu cha Quaran. ( Picha na Tamimu Adam).
Na Tamimu Adam
Wazazi
na walezi wa kiislamu wametakiwa kuenzi na kuihifadhi Quran tukufu
na kuipa heshima ya aina yake kwa kuwahamasisha watoto wao kushiriki
katika mashindano ya kusoma na kuifadhi Quran ili kuwawezesha kufahamu
vizuri uislamu na kuwa muongozo katika maisha yao ya kila siku hapa
dunia na kesho ahera.
Hayo
yalisemwa na Ustaadhi Iddrisa kutoka Kigoma wakati wa mashindano ya
kusoma na kuifadhi qurani yaliandaliwa na Madrasa ya AL-Mustakima
iliyopo mbagala bucha jijini, Dar es salaam ambapo watoto wa kiislamu
takribani kumi (10) wenye umri kati ya miaka sa sita hadi kumi na tatu
wa madrasa nne ambavyo ni Madrasa Tul – Mustakima ya yombo dovya na
mbagala bucha, madrassa Tul- ukutani na madrassa Tul Ismailia ya mtoni
kijichi.
Naye
Mwalimu mkuu wa Madrasa ya AL- mustakima ambayo ndio mratibu wa
mashindano hayo Ustaadhi Hassani Suleimani alisema mashindano hayo
yalishirikisha wanafunzi kumi ambao waligawanywa katika makundi makuu
mawili kundi la kwanza ni wanafunzi watano kutoka vyuo vyote nne ambao
walisoma na kuifadhi juzuu mbili na kundi la pili ni kwa wanafunzi ambao
walisoma na kuifadhi juzuu tano.
Aidha
, aliongeza kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuwafundisha vijana
kusoma na kuhifadhi kitabu cha mwenyezi mungu, kuipenda qurani na
kuitumia katika maisha yao yote pamoja na kuwafundisha maadili ya
kiislamu na maamurisho yake yote kwa waislamu. Aliongeza kuwa
mashindano hayo yalisimamiwa na majaji watatu kutoka mbande ambao kwa
ujumla walikuwa wanaangalia vigezo mbalimbali ikiwemo namna ya kusoma
na kutamka maneno ya quaran kwa usahihi.
Kwa
upande wake Imamu wa Msikiti wa mbagala charambe Sheikh Adam
Mikidadi ambaye alikuwa miongoni mwa majaji wa mashindano hayo alisema
kuwa mashindano yalienda vizuri ambapo yalifanyika kwa kiwango
kilichotarajiwa, washiriki walisoma na kutamka quarani vizuri kabisa na
kuweza kufikia vigezo vya mashindano kwa asilimia 85.
Sheikh
aliwataka washiriki wote kuongeza bidii mwakani ili waweze kufikia
asilimia 100 na kuwa mahiri katika kusoma, kuhifadhi na kukuza uislamu
ndani ya jamii.
Pia
aliwataka wazazi na walezi kuhamasika na kuisoma quaran tukufu ili iwe
muongozo wao katika maisha yao yote na kwa wale wenye uwezo wawe na
tabia ya kujitolewa kudhamini mashindano ya kusoma na kuhifadhi kitabu
cha mwenye mungu.
Washiriki
wa mashindano hayo walipewa zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza
Zahara Mohamed alizawadiwa shilingi laki moja na thelathini kwa kusoma
na kuhifadhi juzuu 5 kati ya juzuu thelathini na wa pili alizawadiwa
fedha taslimu elfu themanini, tano na watatu alizawadiwa shilingi elfu
sitini na tano na wengine walipewa elfu arobaini.
0 comments:
Post a Comment