SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, February 18, 2012

Jeshi La Polisi: Dk. Harrison Mwakyembe Hakupewa Sumu!!

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe baada ya kuugua
Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe Kabla ya Kuugua
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Kamishna Robert Manumba
****
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Kamishna Robert Manumba amesema taarifa za uchunguzi zilizofanywa na Jeshi la Polisi zinaonesha kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe hakupewa sumu.
Manumba alitoa taarifa hiyo wakati wa kujibu maswali ya waandishi wa habari alipokutana nao jana Makao Makuu ya Polisi kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa uhalifu nchini.
Pamoja na mambo mengine, waandishi hao walitaka kujua hatua iliyochukuliwa na Jeshi la Polisi kuhusu madai yaliyotolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta kwamba Mwakyembe alipewa sumu.
Kanumba alisema hata kabla ya madai ya Sitta, Jeshi la Polisi lilikuwa linafanya uchunguzi kuhusu madai ya Dk. Mwakyembe ya kupokea ujumbe wa kutishiwa maisha.
"Kabla Mwakyembe hajaugua na kupelekwa India tulimhoji kuhusu malalamiko aliyowasilisha kwa maandishi kwamba alipokea ujumbe wa kumtishia maisha yake…pia tumeendelea kufanyia kazi tuhuma zinazotolewa na Sitta maana kuna jinai ndani yake,” alisema Manumba.
Alisema katika uchunguzi huo, ofisi yake iliwasiliana na Wizara ya Afya kuomba taarifa za uchunguzi wa kisayansi kama ugonjwa wa Mwakyembe unatokana na kulishwa sumu.
“Hata hivyo taarifa tuliyoipata kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaonesha kuwa ugonjwa uliokuwa unamsumbua Mwakwembe hautokani na kula chakula chenye sumu,” Manumba alisema.
Alisema ofisi yake ikishakamilisha kuandika ripoti ya uchunguzi itaiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.
Waandishi wa habari walipotaka kufahamu kama Waziri Sitta atashtakiwa kwa kutoa habari zisizokuwa na ukweli, Manumba alisema Sheria ndio itaamua ashitakiwe au asishitakiwe. Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM) alikuwa mtu wa kwanza kuibua rasmi shutuma kuwa Dk. Mwakyembe, alikula chakula chenye sumu.
Sitta ambaye ni rafiki na mshirika wa karibu wa Dk. Mwakyembe katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini alitoa kauli hiyo katika mahojiano ya Kituo cha Televisheni cha ITV katika kipindi chake cha dakika 45.
Chanzo: H@ki Ngowi.

0 comments:

Post a Comment