DR.SHEIN AIBUKA KINARA KINYAG'ANYIRO CHA KUWANIA KUGOMBEA URAIS
KISIWANI ZANZIBAR
HATIMAYE MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANAZANIA DR.
ALLY MOHAMED SHEIN AMEIBUKA KIDEDEA KWA KURA 117 NA KUWABWAGA WAPIZANI
WAKE DR. GHALIB BILAL NA WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI
ZANZIBAR SHAMSI VUAI NAHODHA KATIKA KINYAG'ANYIRO CHA KUWANIA KUGOMBEA
URAIS KISIWANI ZANZIBAR.
DR.SHEIN ALIWASHINDA
GHALIB BILAL AMBAYE AMEPATA 54 NA KUSHIKA NAFASI PILI AKIFUATIWA NA
SHAMSI VUAI NAHODHA AMBAYE AMESHIKA NAFASI YA TATU KWA KUPATA KURA 33.
Ushindi wa Dr Shein na matukio mbali mbali ya mkutano wa kamati kuu.
*****************************
Ushindi wa Dr Shein na matukio mbali mbali ya mkutano wa kamati kuu.
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akiwashukuru wajumbe wa Halmashauri kuu
ya taifa CCM kwa kumchagua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM.
Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru akimpongeza
Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya uchaguzi ambapo Dr.Ali Mohamed
Shein aliibuka mshindi katika ugombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya
CCM jana usiku mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimpongeza makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa na
wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuwa mgombea Urais wa Zanzibar
kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika ukumbi wa White house mjini
Dodoma jana usiku.
MKUTANO MKUU WA
CCM LIVE TOKA DODOMA SASA
MWENYEKITI
WA CCM JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIONGOZA MKUTANO MKUU WA CCM HIVI SASA
HUKO DODOMA. FUATILIA MAMBO YOTE LIVE: BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment