Watu Mia Moja Wauwawa Pakistan
Watu mia moja wameuwawa katika
mashambulizi ya mabomu ya kujitoa mhanga katika kijiji kimoja nchini
Pakistan kinachopakana na Afghanistan.
Watu wawili walishambulia kijiji cha Yakaghund
katika mkoa wa Mohmand, na kuyaharibu majengo ya serikali, maduka na
nyumba kadhaa.
Mohmand ni sehemu ya mikoa ya kikabila nchini
Pakistan, ambako Taliban na al Qaeda wako na wanamgambo wengi.
Msemaji wa Taliban alisema kundi lao lilihusika
na mashambulizi hayo.
Msemaji huyo, Ikramullah Mohmand alisema
walikuwa wanalenga mkutano wa maafisa wa serikali na wazee wanaopinga
Taliban kutoka kabila la Anbar Utmankhel.
Taarifa za hapo awali zilisema watu waliofariki
dunia ni 50 na kusema mtu mmoja ndiye aliyefanya shambulizi hilo.
Hata hivyo, maafisa baadaye walisema kwa uchache
watu 102 walifariki dunia na wengine zaidi ya 115 kujeruhiwa.
Miili mingine zaidi ilipatikana kutoka mabaki ya
majengo na wengine walifariki hospitalini kutokana na majeraha.
Mlipuko huo ulitokea karibu na ofisi ya afisa wa
serikali Rasool Khan, ambaye hakuumia.
Wazee wa kikabila walikuwa katika jengo hilo
lakini hawakuumia, kulingana na mkuu wa utawala wa mkoa wa Mohmand Amjad
Ali Khan.
Alisema shambulizi hilo lilionyesha "hali ya
kukata tamaa" ya kundi la Taliban.
Mmoja ya milipuko hiyo iliharibu ukuta wa gereza na kusababisha baadhi ya wafungwa kutoroka, ingawa walioweza kutoroka hawakuwa wanagambo, alisema Rasool Khan.
Mmoja ya milipuko hiyo iliharibu ukuta wa gereza na kusababisha baadhi ya wafungwa kutoroka, ingawa walioweza kutoroka hawakuwa wanagambo, alisema Rasool Khan.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa miongoni
mwa waliouwawa ni wanawake na watoto.
Jimbo la Mohmand limekuwa uwanja wa mapambano makali kati ya jeshi la Pakistan na wanagambo wa Taliban. bbc swa
Jimbo la Mohmand limekuwa uwanja wa mapambano makali kati ya jeshi la Pakistan na wanagambo wa Taliban. bbc swa
0 comments:
Post a Comment