Rais Lula da Silva wa Brazil aahidi kufuta madeni kwa nchi za Kiafrika
Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil amesema kuwa, analazimika kukata safari yake barani Afrika, kwa minajili ya kukagua maeneo yaliyoathirika na mafuriko huko kaskazini mashariki kwa Brazil. Rais Lula da Silva amezungumza na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na pande hizo mbili zimesisitiza juu ya kuimarisha zaidi mashirikiano ya kibiashara. Akizungumza kwenye mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya Brazil na Afrika Kusini, Rais Lula da Silva amesema kuwa, Brazil ina azma ya kufuta madeni yote inayozidai nchi za Kiafrika katika siku za usoni. Hii ni safari ya mwisho kwa Rais wa Brazil kulitembelea bara la Afrika kabla ya kumaliza vipindi vyake viwili vya uongozi nchini humo. Hapo mwanzo ilipangwa kuwa, Rais wa Brazil angelishuhudia mechi ya fainali ya kombe la dunia, lakini kutokana na mafuriko yaliyotokea kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na kupelekea watu wasiopungua 50 kupoteza maisha yao, imemfanya kiongozi huyo erejee nyumbani. Rais Lula da Silva amezitembelea nchi za Cape Verde, Equatorial Guinea, Kenya, Tanzania, Zambia na hatimaye Afrika Kusini.
****************************
Musyoka: Kenya inaunga mkono Iran katika utumiaji wa nishati ya nyuklia |
Kalonzo Musyoka Makamu wa Rais wa Kenya amesema kuwa, utumiaji wa nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani ni haki ya nchi zote, ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Akizungumza na Muhammad Jawad Muhammadzadeh Makamu wa Rais na Mkuu wa Taasisi ya Hifadhi ya Mazingira ya Iran, Musyoka amekosoa vikali misimamo ya kindumakuwili ya nchi za Magharibi na kuongeza kuwa, nchi zote duniani zina haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani, ikiwemo Iran. Aidha Makamu wa Rais wa Kenya amesema kuwa, vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Baraza la Usalama dhidi ya Iran vinavyotokana na mashinikizo ya Marekani si vya kiadilifu na kusisitiza juu ya kuimarishwa mashirikiano kati ya Tehran na Nairobi katika sekta za biashara na uchumi. Naye Makamu wa Rais wa Iran na Mkuu wa Taasisi ya Hifadhi ya Mazingira amesema kuwa, safari ijayo ya Rais Mwai Kibaki wa Kenya mjini Tehran itazidi kuimarisha mashirikiano ya pande hizo mbili. |
0 comments:
Post a Comment