SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 7, 2012

Steven Kanumba Muingizaji wa Bongo Movies Amefariki Dunia Usiku wa Kuamkia Leo!!

Picha juu ni Steven Kanumba Muingizaji wa Bongo Movies ambae amefariki dunia usiku wa kuamkia Leo.
KWA MUJIBU WA MDOGO WA MAREHEMU STEVE KANUMBA, ALISEMA KUWA ELIZABETH MICHAEL MAARUFU KAMA LULU ALIKUJA NYUMBANI KUKAWA NA KAUGOMVI AMBAPO WAKAINGIA CHUMMBANI WAKIWA HUKO BAADA YA MUDA,LULU ALITOKA NA KUMUITA YEYE KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA, YE ALIPOENDA AKAMKUTA KAANGUKA NDIO AKAENDA MUITA DAKTARI WA KANUMBA AMBAPO ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU, LAKINI HADI TUNAVYOONGEA LULU YUKO POLISI OSTERBAY KWA AJILI YA MAHOJIANO NA POLISI.


ELIZABETH MICHAEL (MAARUFU KAMA LULU)
Inasemekana Lulu aligombana na marehemu Kanumba ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wake baada ya kukutwa akiongea na mwanaume mwingine kitendo ambacho kilimuudhi marehemu.. Lulu anasemekana kumsukuma marehemu na ndipo alianguka na umauti kumfikia jana usiku...
Chanzo: BOFYA
HABARI TULIZOPATA USIKU WA KUAMKIA LEO NA KUTJHIBITISHWA ASUBUHI HII NI KWAMBA MWIGIZAJI MAARUFU NCHINI STEVE KANUMBA (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO NYUMBANI KWAKE SINZA 'VATICAN' JIJINI DAR ES SALAAM.
HABARI ZA AWALI AMBAZO HAZIJATHIBITISHWA ZINASEMA UMAUTI UMEMKUTA MAREHEMU KANUMBA BAADA YA KUTOKEA TAFRANI KATI YAKE NA MWANDANI WAKE WAKIWA WANAJIANDAA KUTOKA KWENDA OUT MILANGO YA SAA SABA USIKU. KATIKA PURUKUSHANI HIO MAREHEMU ALIGOTA UKUTA NA KUZIRAI BAADA YA KUUMIA KISOGONI.
HABARI ZAIDI ZITAFUATA BAADA YA KUTHIBITISHA KILA KITU. MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU SINZA 'VATICAN' AMBAKO NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WAMEKUSANYIKA HIVI SASA
KUJIANDAA NA MIPANGO YA MAZISHI. MWILI WA MAREHEMU UKO HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.
MOLA AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU - AMINA.
GLOBU HII IMEPOKEA HABARI HIZI KWA MSTUKO NA MAJONZI MAKUBWA
-----
HISTORIA YAKE
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.
Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.

HII NDIYO MUVI MPYA ALIYOTUACHIA MAREHEMU STEVEN KANUMBA IITWAYO KIJIJI CHA TAMBUA HAKI

0 comments:

Post a Comment