SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, November 3, 2013

Vipande 700 vya meno ya Tembo vimekamatwa maeneo ya Mikocheni - DSM



Zaidi ya vipande 700 vya meno ya Tembo ambavyo vinakadiriwa kuwa ni zaidi ya tembo 200 kama wangekuwa hai vimekamatwa katika maeneo ya mikocheni


Raia wa China wamekamatwa jijini Dar es Salaam maeneo ya Mikocheni  wakiwa na shehena ya vipande 700 vya meno ya tembo.
Wakazi wa eneo hilo wanaowafahamu Wachina hao wamesema huwa wanawaona wakiuza ndimu na vitunguu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Kaghasheki amesema inakadiriwa kuwa ni zaidi ya tembo 200 waliouawa ili kupata meno hayo. Akasema amemweleza mmoja wa Wachina hao kuwa ingelikuwa amekamatwa nchini kwao China, hukumu ambayo ingempasa ni kifo.
Waziri pia alisema anahisi huenda watu hawa wakawa wanafahamu ama kuhusika na moja ya makontena yaliyokamatwa nchini China yakiwa na meno ya tembo

0 comments:

Post a Comment