SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, July 31, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA MAPAMBANO YA NGUMI YALIYOCHEZWA IDDI PILI MANZESE

Bondia Sadick Nuru (kushoto) akioneshana umwamba na Baraka Mchonge wakati wa pambano lao lililofanyika Siku ya Iddi Pili kwenye Ukumbi wa Manyara Park Manzese jijini Dar es Salaam.Katika pambano hilo Sadick, alishinda kwa pointi.
Bondia Steven Kobelo (kushoto) akipambana na Karim Ramadhani. Katika pambano hilo hakupatikana mbabe. 

Mabondia Joseph Gili(kushoto)akioneshana umwamba wa na Ibrahimu Tamba Katika pambano hilo Tamba alishinda kwa K/O raundi ya nne. 
Bondia Julius Kisalawe (kushoto) na Ramadhani Kumbele wakichapana wakati wa pambano lao la kuwania ubingwa wa 
 TPBC uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam Kumbele alishinda kwa point na kufanikiwa kuchukua ubingwa huo. Picha na Super D
Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' kulia akimvisha mkanda wa ubingwa bondia Ramadhani Kumbele baada ya kumdunda Julius Kisalawe kwa point kushoto ni Mwamuzi Ally Bakari.

KIKOSI CHA TAIFA STARS CHATUA SALAMA JOHANNESBURG KUJIANDAA KUWAKABILI MSUMBIJI JUMAPILI HII-MAPUTO

Na Boniface Wambura, Johannesburg
Kikosi cha Taifa Stars kimewasili salama jana (Julai 30 mwaka huu) hapa Johannesburg kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo, Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili ya wiki hii.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi mara mbili leo- asubuhi na jioni kwenye uwanja wa Bedfordview Country Club. Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla ya baadaye jioni kuanza safari ya Maputo.
Wakati huo huo, Balozi wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia Msuya baadaye leo jioni atazitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa Johannesburg kusalimia wachezaji.
Serengeti Boys yenyewe ipo hapa tangu Julai 27 kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu).

Boniface Wambura
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 
KWA MAWASILIANO ZAIDI BOFYA NAMBA HIIB +27609217526

Tuesday, July 29, 2014

NAWATAKIA EID MUBARAK NA KILA LA KHEIR WADAU WOTE WA ALLYSHAMS BLOG POPOTE PALE DUNIANI MUNGU AWABARIKI

http://img.xcitefun.net/users/2013/07/328970,xcitefun-happy-eid-2013-12.jpg 
http://worldrapid.com/wp-content/uploads/2013/08/2013-Eid-Mubarak-messages-SMS-Wishes.jpg

MSANII WA BONGO MOVIE ESTER KIAMA AFUTURISHA WASANII WENZAKE JIJINI DAR

Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama leo alifuturisha wasanii, ndugu,jamaa na marafiki zake ikiwa ni ishara ya kumkumbuka marehemu mama yake mzazi ambaye alishatangulia mbele ya haki. Akitoa shukrani zake kwa waalikwa, alisema ameona vyema kuandaa chakula cha pamoja ili waweze kumuenzi mama yao mzazi kwa vile alipenda sana watu hasa kukutana na kupata chakula pamoja.

UGAIDI HAUNA UHUSIANO NA DINI ASEMA SHEIKH ATAKA VIONGOZI WA DINI ZOTE KUKUTANA NA SERIKALI KUTAFUTA MFADHILI WA UGAIDI NCHINI

kaimu sheikh wa  mkoa  wa  Iringa  Abubakar Chalamila
Waumini  wa  dini ya kiislamu mjini  Iringa  wakiwa katika ibada ya idd uwanja wa Samora  leo

Swala ya Eid El Fitr kitaifa yaswaliwa kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar leo



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati),Sheikh Mkuu,Issa Shaaban Simba,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum wakijumuika na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam kwenye Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.

Rais Kikwete aandaa futari kwa yatima, walemavu wa ngozi na watoto waishio kwenye mazingira magumu ikulu Dar es salaam

Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni

Monday, July 28, 2014

Abdallah Bin Klebu (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji. Picha ya Maktaba.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa Yanga, Beno Njovu alisema uamuzi wa kuvunja Kamati ya Utendaji na kuteua wajumbe wapya ni kwa mujibu wa azimio namba nne la mkutano wa wanachama kuhusiana na mabadiliko ya katiba yaliyofanyika Januari 20, 2013.   Njovu alisema katika mkutano huo, wanachama wa Yanga walimpa mamlaka mwenyekiti na makamu wake kuvunja au kuteua wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kamati nyingine za klabu hiyo.
Alisema wajumbe wa sasa wa Kamati ya Utendaji watamaliza muda wao Julai 31 na wapya wataanza kazi Agosti Mosi.  “Uamuzi huu ni kwa mujibu wa Ibara ya 28 kifungu kidogo cha kwanza cha katiba ya klabu. Hivyo ni uamuzi sahihi ambao mwenyekiti na kamati yake wameupitisha. Tunawashukuru wajumbe waliotumikia klabu hiyo kwani bado ni wanachama wetu,” alisema Njovu.   Wajumbe wapya walioteuliwa na Manji na Sanga ni Abubakari Rajabu, ambaye amepewa kazi ya kusimamia mradi wa Jangwani City, Sam Mapande (sheria na utawala bora), George Fumbuka (uundwaji wa shirika), Wazir Barnabas (vibali vya hatimiliki na mahusiano na wafadhili) na Abbas Tarimba, ambaye atashughulikia mipango na uratibu.
Wengine katika orodha ya wajumbe wapya ni Isaac Chanji na Seif ‘Magari’ Ahmed (uendeshaji wa michezo), Musa Katabalo (mauzo ya bidhaa), Mohamed Bhinda (ustawishaji matawi), David Sekione (uongezaji wa wanachama) na Mohamed Nyenge, ambaye atashughulikia masuala ya utangazaji wa habari, taarifa na matangazo.  Njovu alifafanua kuwa wajumbe wa kamati hiyo mpya pia watakuwa na kazi ya kusimamia kamati ndogo ndogo za klabu hiyo. Alisema Mapande atasimamia Kamati ya Maadili, Nidhamu na Uchaguzi wakati Fumbuka na Barnabas watasimamia Kamati ya Uchumi na Fedha, huku Seif Magari na Isaac Chanji wakisimamia Kamati ya Mashindano, Soka la Vijana na Wanawake na Ufundi.  Akizungumzia kutoswa kwake katika Kamati ya Utendaji ya Yanga, Bin Kleb alisema miezi miwili iliyopita aliwaomba viongozi wasimteue kwenye Kamati ya Utendaji.
Habari kwa hisani ya http://www.mwananchi.co.tz/

Sunday, July 27, 2014

Tanzania National Defence College's Second Course 2013/14 Valedictory function

 The Commander-in-Chief President Jakaya Mrisho Kikwete is received by the Chief of Defence Forces General Davis Mwamunyange as he arrives to officiate at the Tanzania National Defence College's Second Course  2013/14 Valedictory function at Kunduchi in Dar es salaam on Saturday July 26, 2014. Looking on centre is the College Commandant Lieutenant General  (Engr) Charles  Lawrence Makakala
 The Commander-in-Chief President Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with the Minister for Defence and National Service Dr Hussein Mwinyi as he arrives to officiate at the Tanzania National Defence College's Second Course  2013/14 Valedictory function at Kunduchi in Dar es salaam on Saturday July 26, 2014. Looking on centre is the College Commandant Lieutenant General Jamaes Makakala
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akipimwa kabla ya kuchangia damu katika zoezi lilioendeshwa na Shrika la Red Cross katika kuchangia damu Mkoani Rukwa. Kumekuwepo na uhaba mkubwa wa damu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na vituo vingine uhaba ambao unafikia nusu kwa nusu ukilinganisha kiasi kinachopatikana na mahitaji yaliyopo. Uhaba huo umesababishwa na muamko hafifu wa wananchi kuchangia damu kutokana na hofu inayosababishwa na dhana potofu kuwa uchangiaji damu una madhara kwa mchangiaji. Madaktari hao wa Hosptali Kuu ya Mkoa pamoja na watumishi wengine wa Serikali waliamua kujitolea ili kuonyesha mfano kwa wananchi waweze kuondokana na hofu hiyo waweze kujitokeza kuchangia damu kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji huduma hiyo muhimu.
Baadhi ya madaktari wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa wkichangia damu.
Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Esther Kasegezya akichangia damu katika zoezi hilo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Samwel Marwa akipatiwa vipimo muda mfupi kabla ya kuchangia damu.
Dkt. Marwa akichangia damu.
Mchangiaji baada kutoa damu hupata viburudisho ikiwemo vinywaji baridi na biskuti maalum.
Sehemu ya damu iliyokuwa imechangiwa katika zoezi hilo.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)
NA MTAA KWA MTAA

DIAMOND ASHINDA TUZO ZA AFRIMMA ZILIZOFANYIKA MAREKANI

Screen Shot 2014-07-27 at 9.43.50 AMZinaitwa African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo.

Mama Kikwete ahimiza wanafunzi wa kike wa vyuo vya ualimu kuvaa mavazi ya heshima

Na Anna Nkinda - Maelezo,  Nachingwea

Wanafunzi wa kike wa vyuo vya ualimu nchini wametakiwa kuvaa mavazi  nadhifu  yanayoendana na maadili ya kazi yao  ili wanafunzi na jamii inayowazunguka ijifunze  kutoka kwao kwani wao ni kioo cha jamii.

Mwito huo umetolewa  hivi karibuni  na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na baadhi ya wanafunzi wa kike  wa chuo cha Ualimu Nachingwea mara  baada ya kumalizika kwa futari aliyoiandaa kwa ajili ya viongozi wa wilaya iliyofanyika  chuoni hapo. 

UZINDUZI WA KAMPENI YA SHUGA REDIO MKOANI IRINGA WAFANA SANA

  DSC_0145
 Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumba akitoka kukagua jukwaa lenye hadhi ya kimataifa la Ebony FM kwenye uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika jana kwenye viunga vya Samora mkoani Iringa.
DSC_0455
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Tosamaganga wakiwasili kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa kushuhudia uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio inayowalenga vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 iliyozinduliwa rasmi jana mkoani humo.

SERENGETI BOYS KWENDA AFRIKA KUSINI KESHO

Msafara wa watu 25 wa kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) unaondoka kesho (Julai 28 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Kusini.

Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Mshindi atacheza raundi ya mwisho ya michuano hiyo ya Afrika na mshindi wa mechi kati ya Misri na Congo Brazzaville.

Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwakani nchini Niger.

Wachezaji wanaounda kikosi cha Serengeti Boys katika msafara huo utakaoondoka saa 2 usiku kwa ndege ya Fastjet ni Abdallah Jumanne Shimba, Abdulrasul Tahil Bitebo, Abutwalibu Hamidu Msheri, Adolf Mtsigwa Bitegeko, Ally Aziz Mnasi, Ally Shaban Mabuyu na Athanas Enemias Mdamu.

Wengine ni Badru Haji Othman, Baraka Yusuph Baraka, Issa Backy Athuman, Juma Ally Yusuph, Kelvin Longnus Faru, Martin Kiggi Luseke, Metacha Boniface Mnata, Mohamed Mussa Abdallah, Omary Ame Omary, Omary Natalis Wayne, Prospal Alloyce Mushin na Seif Said Seif.

Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu Hababuu Ally Omary akisaidiwa na Stewart John Hall (Mshauri wa Ufundi), Peter Manyika (Kocha wa makipa), Richard Yomba (Daktari), na Edward Venance (Mtunza vifaa).
 
Msafara wa timu hiyo itakayorejea nyumbani Agosti 4 mwaka huu unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Khalid Mohamed Abdallah.

NSSF YAKUTANA NA KUFTURI PAMOJA NA WASTAAFU WAKE MKOA WA TANGA

Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Maryam Muhaji akizungumza jambo katika hafla ya kufuturisha wastaafu iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach,Mkoa wa Tanga jana. 
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Alhaji Juma Luwuchu akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
Kaimu Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Tanga, Emmanuel Masika akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika mkoani Tanga.
Mmoja wa wastaafu akitaka ufafanuzi kutika kwa viongozi wa shirika hilo kuhusu huduma za shirika hilo.
Mstaafu wa NSSF, Edith Lumeya akiuliza swali kuhusu malipo ya wastaafu.
Mstaafu wa NSSF, Muni Hussein Ally  akiuliza swali.

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA AANDAA FUTARI NYUMBANI KWAKE DAR ES SALAAM

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum alipowasili kwenye makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda (nyuma yao) Oysterbay jijini Dar es salaam kwa ajili ya Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na wa pili kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova
 Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakijumuika na waumini wengine katika Swala ya Magharibi katika  makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda Oysterbay jijini Dar es salaam alikoandaa Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013

TAMKO LA JUKWAA KUHUSU BUNGE MAALUM LA KATIBA LINALOANZA MJINI DODOMA AGOSTI 5, 2014


 Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko kuhusu Bunge la Katiba litakaloanza Agosti 5, 2014 ambapo walishauri Bunge hilo likae wiki mbili badala ya miezi miwili kama ilivyopangwa ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za Umma. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Kamati na Uongozi Jukata Omar Ali Omar,  Meneja Habari na Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Kenny Ngomuo, Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda na  Mratibu wa Jukata, Diana Kidara.
 Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda, akisoma tamko hilo.
 Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. Picha na Cathbert Kajuna

SIMANZI ZAENDELEA KUTAWALA NDANI YA NYUMBA YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) MARA BAADA YA MSHIRIKI MWINGINE KUAGA SHINDANO

Majaji wa shindano la TMT wakimsikiliza kwa makini Mshiriki wa TMT, Mwanaafa Mwinzago (anayeonekana kwenye runinga mbele) wakati akijielezea kabla ya filamu fupi aliyoshiriki kuonyeshwa ili majaji waweze kutoa hukumu kwa washiriki wa kundi hilo

Saturday, July 26, 2014

LOOSE WEIGHT NOW, ASK ME HOW!


RATIBA YA MABONDIA WA TANZANIA WANAOWAKILISHA TAIFA KATIKA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA SCOTLAND (NDONDI)

Hatimaye ratiba ya mchezo wa ngumi kwa mashindano ya Jumuiya ya Madola imetolewa leo tarehe 24/07/14 baada ya zoezi la kupima uzito na afya lililofanyika kuanzia saa 2.00 hadi saa 4.00 Asubuhi kwa saa za Scotland, kwa mabondia na waamuzi wote wanaotegemea kushiriki mashindano hayo`1.

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa mashindanoo yataanza  tarehe 25/07/14 na yatamalizika tarehe 02/08/14.katika ukumbi wa Secc (Hall 4A) na inaonyesha kuwa captain wa timu ya Tanzania Selemani kidunda ndiye atayeanza kupeperusha bendera ya taifa na hatiaye kufatiwa na mabondia wengine kama ifuatavyo:-

Tarehe 25/07/14 saa 1.45 Jioni  (69) kg  
        Kehinde Ademuyiyiwa (Nigeria) v/s Selemani Kidunda (Tanzania)

Tarehe 26/07/14 saa 7.20 Mchana (60) kg
                    Jessie Lartey (Ghana) v/s Nasser Maffuru ( Tanzania)
                                      Saa 1.00 Jioni (64) kg
        Stevin Thanki (Malawi) v/s Fabian Gaudensi (Tanzania)

Tarehe 27/07/14 saa 12.45 Jioni( 52) kg
                         Bye v/s Ezra Paul ( Tanzania)
                                               Saa 1.40 Jioni (8I)kg
                     Mohamed Hakimu (Tanzania) v/s Sumit Sangwan (India)

Tarehe 28/07/14 saa 7.25 Mchana) (56)kg
        Bashiri Nasir (Uganda) v/s Emilian Patrick (Tanzania)
                                               Saa 1.35 jioni (49) kg
                  Paddy Barnes( Northern Ireland) v/s Hamed Furahisha (Tanzania) 

Taarifa hizi zimeletwa na 

Makore mashaga
KATIBU MKUU.

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA LEO

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kasimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwela ngao kwenye mnara wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo. Wengine ni  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Waziri Mkuu Mzengo Pinda leo Julai 25, 2014
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Frederick Sumaye  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo.Wengine toka kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe Mohamed Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar  Mhe omar  Othman makungu leo Julai 25, 2014
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiamkiana na wazee wa Tanzania Legion waliopigana katika vitra kuu ya dunia ya pili  waliohudhuria  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani  ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014.Picha na IKULU