Na Boniface Wambura, Johannesburg
Kikosi
cha Taifa Stars kimewasili salama jana (Julai 30 mwaka huu) hapa
Johannesburg kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo,
Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili ya
wiki hii.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi mara mbili
leo- asubuhi na jioni kwenye uwanja wa Bedfordview Country Club.
Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla
ya baadaye jioni kuanza safari ya Maputo.
Wakati
huo huo, Balozi wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia Msuya baadaye leo
jioni atazitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa
Johannesburg kusalimia wachezaji.
Serengeti
Boys yenyewe ipo hapa tangu Julai 27 kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika
Kusini itakayochezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu).
Boniface Wambura
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
KWA MAWASILIANO ZAIDI BOFYA NAMBA HIIB +27609217526
0 comments:
Post a Comment