SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 29, 2013

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZ​I WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

PIX 1 f3694
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto)akimpokea Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi cha siku tatu kinachofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. Katika Hotuba yake ya ufunguzi, Ntunguja aliwaomba watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane vizuri na watumishi wao ili kuleta mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
PIX 2 8e6ee
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akizungumza na wajumbe wa baraza hilo kabla ya kufungua kikao cha siku tatu kinaofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edson Nyinyimbe. Wa pili kushoto ni Venance Ntiyalundura, Katibu wa tawi hilo. Katika kikao hicho Ntunguja aliwaomba watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane vizuri na watumishi wao ili kuleta mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
PIX 3 abd9f
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya kufungua mkutano wa wafanyakazi wa siku tatu unaofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya.

 Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiimba nyimbo ya mshikamo daima kabla ya mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja (hayupo pichani) kufungua kikao cha baraza hilo kinachofanyika katika Hoteli ya Paradise, jijini Mbeya.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja (wa tano kutoka kushoto waliokaa), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa tano kulia waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi (wanne kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa idara wa wizara hiyo na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya Kikao cha siku tatu cha baraza hilo kufunguliwa katika Hoteli ya Paradise, jijini Mbeya leo.
 Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

0 comments:

Post a Comment