SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 29, 2013

Neno La Leo; Ng'ombe Wa Serikali Huzikwa Na Ngozi Yake...!

58506_10201565008299820_776742125_n_66934.jpg
Ndugu zangu,
Katika kitabu chake; The Flags Changed At Midnight- Mwandishi na ambaye alikuwa DC wa Mkoloni kuanzia 1951-62, Bw. Michael Longford anaelezea jinsi Serikali ya Mwingereza ilivyokuwa makini.
Anasema, kuwa aliyethubutu kuchezea shilingi ya Serikali alijuta kuzaliwa.
Naam, kila kunapokucha, kuna Watanzania wenzetu mahali fulani wenye kupanga ya kutafuna mamilioni ya fedha za Wananchi. Ni wenye kupanga pia matumizi mabaya ya fedha za Wananchi.
Na kesho kutwa itaingia kama vile hakuna kilichotokea jana yake.
Naam, ng'ombe wa Serikali huzikwa na ngozi yake. Ni nani anayejali? Maana, kama ng'ombe ni wa wakoi, basi, akifa, utahakikisha walau unachuna ngozi yake, ili walau uambulie senti kidogo!
Ni Neno la Leo.
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam

0 comments:

Post a Comment