SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, February 3, 2014

SIKU YA SHERIA DUNIANI MWAKA 2014

    Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akiwaongoza Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania katika Maandamano ya kuadhimisha Siku ya Sheria nchini leo asubuhi katika viwanja vipya vya Mahakama vilivyopo Mtaa wa Chimala karibu na Southern Sun Hotel.
   Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika Sherehe za Siku ya Sheria nchini.
      Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Augustine Ramadhan  akiwa pamoja na Viongozi wengine wastaafu wa Mahakama katika sherehe hizo zilizofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyeji wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman mara alipowasili katika viwanja hivyo kama Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo.

 Ukaguzi wa gwaride kuashiria uzinduzi rasmi wa Shughuli za Mahakama kwa mwaka 2014
   Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa na Majaji wenzake wakipokea heshima ya gwaride katika sherehe hizo katka viwanja vya Botanical Ocean road jijini Dar es salaam leo asubuhi.
NA MICHUZI MATUKIO

0 comments:

Post a Comment