SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, February 3, 2014

MAWAZIRI WALUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KUELEZEA MAENDELEO YA ELIMU.


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali zanzibar, Ali Juma Shamuhuna (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na Waziri wa Elimu na Ufundi wa Tanzania Bara, Shukuru Kawambwa, mkutano uliowashirikisha pia maofisa kutoka Wizara hizo mbili, ulifanyika kwenye makao makuu ya Wizara ya Elimu mjini Zanzibar jana (kushoto) ni Waziri Shukuru Kawambwa.
Mawaziri Ali Juma Shamuhuna na Shukuru Kawambwa wakiongoza mkutano ulowashirikisha maofisa kutoka Wizara hizo jana.
Waziri wa Elimu na Ufundi wa Tanzania Bara, Shukuru Kawambwa akizungumza kwenye kikao hicho jana. Picha na Martin Kabemba.

Story by: Donald Martin Kabemba.

Waziri wa Elimu na Ufundi, Shukuru Kawambwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna kwa pamoja wamekutana kujadili mwenendo wa elimu Tanzania na kuchambua matokeo ya Kidato cha nne hususani viwango vya kufaulu na kufeli na hatimae kuwasilisha taarifa ya mkutano wao kwenye Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Mapinduzi Zanzibar.

Mawaziri hao walikutana jana mjini Zanzibar na kuongea na waandishi wa habari kuhusu maendeleo na mafanikio ya elimu Tanzania baada ya matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka juzi ( 2011/2012) Waziri Shamuhuna alisema kwa upande wa Zanzibar Wizara yake imejizatiti kuhakikisha vitendo vya udanganyifu katika mitihani vinapungua kwa kutafuta kasoro zilizojitokeza mwaka juzi na kuzirekebisha.

"Tumekuwa tukizungumza na mabaraza ya mitihani katika shule mbalimbali ili kuhakikisha hatutarejea pale tulipofanya makosa." Alisema Shamuhuna.

Naye Mheshimiwa Kawambwa amesema baada ya kikao hicho watawasilisha taarifa maalumu kwa mabaraza ya mawaziri ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Lakini pia Waziri huyo amesifu ushirikiano uliopo baina ya Wizara hizo mbili.

" Ushirikiano wetu unazidi kukua siku hadi siku,hili ni jambo zuri kwa maendeleo ya elimu kwa nchi yetu" Alisema Kawambwa.

Wizara hizo mbili zimekuwa na kawaida ya kukutana kabla na baada ya mitihani ya Taifa ili kufanya tathmini ya mitihani hiyo.
Mwisho.
CHANZO BOFAYA HAPA

0 comments:

Post a Comment