SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 29, 2010

Obama afurahishwa na maafikiano ya kutosambaa silaha za kinuklia

Rais Barack 
Obama  akitembea  kuelekea  mahali  anapozungumza  na  waandishi  habari
  katika  ikulu  ya  Marekani White House.
 Rais Barack Obama akitembea kuelekea mahali anapozungumza na waandishi habari katika ikulu ya Marekani White House. 
Rais Barack Obama amefurahishwa na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa umoja wa mataifa yanayohuzu kuzuwia kusambaa kwa silaha za kinuklia
Rais Barack Obama amefurahishwa na makubaliano yaliyoafikiwa katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa, kuhusiana na mkataba wa kuzuia kusambaa kwa silaha za nyuklia. Hata hivyo Obama alipinga vikali, kile alichokitaja ni kuilenga Israel, katika mkutano uliopangwa kufanyika mwaka  2012, na kuyaleta pamoja mataifa yote ya Mashariki ya Kati, ili kuondolea mbali kitisho cha silaha za nyuklia katika Mashariki ya Kati. Mataifa matano  yanayomiliki silaha za Nyuklia, na ambayo yametia saini mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha hizo, yalikubaliana kuchukua hatua zaidi kuzuia tishio la silaha za nyuklia duniani. Mataifa hayo yanayoongozwa na Marekani, Urusi, China, Ufaransa na Uingereza- yote yameridhia pendekezo la kupunguza zana zao za nyuklia.  Hatua hii sasa inaiwekea mbinyo zaidi Israel, pamoja na India, Pakistan na Korea Kaskazini- mataifa matatu ambayo yamekataa kutia saini mkataba huo wa kusambaa kwa silaha za nyuklia.

Watu wenye silaha washambulia misikiti na kuua watu 80 Lahore
Sample ImageHabari kutoka Pakistan zinasema kuwa watu wenye silaha wamewavamia waumini wa Kiislamu katika msikiti mmoja mjini Lahore Pakistan na kuwaua watu wasiopungua 80. Inaripotiwa kuwa mamia ya watu pia wanazuiliwa mateka na genge hilo. Duru za habari zinasema kuwa shambulio hilo limetokea mapema leo wakati wa swala ya Ijumaa katika misikiti kadhaa mjini Lahore. Inasemekana kuwa magaidi hao walitumia maguruneti pamoja na silaha zingine hatari kutekeleza shambulio hilo. Polisi imeanzisha uchunguzi ili kuwakamata waliohusika.
Raila Odinga Waziri Mkuu wa Kenya akutana na Waziri Mkuu wa Uingereza 
Mei 28 2010


Sample Image David Cameron Waziri Mkuu wa Uingereza ameishukuru serikali ya Kenya kutokana na juhudi zake za kupambana na maharamia kwenye pwani ya Somalia. Akizungumza na Raila Odinga Waziri Mkuu wa Kenya mjini London, Cameron ameongeza kuwa London inataka kuimarisha zaidi mashirikiano yake na Kenya katika nyanja zote. Hadi sasa Kenya inawashikilia zaidi ya maharamia mia moja na inakusudia kuwafikisha wahalifu hao mahakamani. Matamshi hayo yametolewa katika hali ambayo mwezi uliopita Kenya ilitangaza kuwa inakusudia kusimamisha shughuli zake katika maji ya pwani ya Somalia kutokana na kutopata msaada wa kutosha kutoka jamii ya kimataifa katika uwanja huo. Waziri Mkuu wa Uingereza leo pia anatarajiwa kukutana na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria na Rais Yoweri Museveni wa Uganda. 
Kiswahili Radio

0 comments:

Post a Comment