
Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila akionyesha picha za
X-Ray alizopigwa baada ya kupewa kipigo na watu wanaodaiwa kuwa ni
wakazi wa Kurasini alipokwenda kuwahamisha Ijumaa iliyopita. Picha na
Joseph Zablon
--
Kiongozi wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher
Mtikila amenusurika kifo na mtu mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la
Mikidadi, ambaye yupo mahututi katika Hospitali ya Temeke, baada ya
kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa na mzozo wa ardhi eneo la Kurasini,
jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Mtikila alikumbwa na mkasa huo Ijumaa
wiki iliyopita baada ya kufika katika eneo hilo kwa nia ya kutaka
kuwaondoa watu hao wa familia tatu tofauti ambao wanaishi katika eneo
hilo.
Kipigo hicho ambacho kimemsababishia majeraha ya
kisogoni na hata kushonwa nyuzi tatu kichwani, kuvimba usoni na maumivu
makali mwilini yalitokana na kipigo kutoka kwa familia mbili tofauti
zinazoishi katika eneo hilo ambao wanapinga kuhama.
Kwa habari zaidi Bofya na Endelea......===>>>
0 comments:
Post a Comment