SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, February 3, 2014

ASKARI POLISI WATANO WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA GARI WAAGWA MKOANI DODOMA TAYARI KWA MAZISHI

 Miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ikiwa imebebwa.
 Miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ya kugongana uso kwa uso na basi la Mohamed Trans.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME akizungumza kwa Masikitiko wakati wa kuaga miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME akiongoza waombolezaji kuaga miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari.
 Waombolezaji.
Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ya kugongana uso kwa uso na basi la Mohamed Trans wameagwa leo Mkoani Dodoma tayari kwa mazishi.

Akiongea kwa masikitiko Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewashukuru watu waliojitokeza kuungana pamoja kuaga miili ya Askari hao.

Pia amewataka madereva wote kuwa waangalifu wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kujitokeza za namna hii.

0 comments:

Post a Comment