Obama: Nitaiunga India kupewa kiti UN.
Obama akiwa ziarani India
Rais Barack Obama ametangaza nia yake ya kuiunga mkono India katika kupigania kiti cha kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa.
Katika hotuba yake kwa bunge la India baada ya kumalizika ziara yake ya siku tatu nchini humo, Obama aliisifu India kwa yale imefikia kimaendeleo na kusema kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utakuwa wa manufaa kwa nchi zote mbili.
Katika suala la dharura zaidi, Obama aliiomba India ichukue msimamo thabiti katika kulinda haki za binadamu kwa nchi kama Burma. Alisema India mara kwa mara imekuwa ikiepuka kuwakemea wanaokosea, lakini amesistiza kuwa kuwatetea wasio kuwa na uwezo kama Burma, sio kuingilia masuala ya ndani ya nchi husika bali ni kutetea misingi ya demokrasia.
Rais Obama alisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya nchi yake na India.
Akizungumzia wanahabari, pamoja na waziri mkuu Manmohan Singh, Obama alisema kuwa uhusiano kati ya India na Marekani una umuhimu kwa dunia.
0 comments:
Post a Comment