Tangazo likipita kwenye big screen.
Kikosi cha Mbeya City
Kamisaa,Marefa pamoja na Manahodha wa timu zote mbili.
Mshambuliaji
machachari wa timu ya Yanga,Mrisho Ngassa (17) akichuana vikali kuwania
mpira na Beki wa Timu ya Mbeya City,Deogratias Julius wakati wa
mtanange wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.Dakika 90 za mchezo zimemalizika hivi
punde na Yanga imeshinda kwa Bao 1-0 lililotiwa kimiani na Mrisho
Ngassa,dakika ya 15 ya mchezo kipindi cha kwanza.
Beki wa Timu ya Mbeya City,Deogratias Julius akijiandaa kuondosha hatari iliyokuwa imekwenda langoni kwao.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga,Haroun Niyonzima pamoja na Beki wa Mbeya City,Yussuf Abdallah wakiwania mpira,wakati wa
mchezo wao wa marudiano katika mzungunguko wa pili wa Ligi kuu Tanzania
Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
David Luhende akimtoka beki wa Timu ya Mbeya City.
Mashabiki wa Mbeya City wakiendelea kuishangilia timu yao.
Mbuyu Twite wa Yanga akiangalia nani na kumpatia pasi wakati wa mtanange wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao la kwanza.
Mashabiki wa timu zote mbili.
0 comments:
Post a Comment