Mwenyekiti
wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia Wananchi na
Wanachama wakereketwa wa chama hicho,mapema leo jioni kwenye kilele cha
maadhimisho ya kusherehekea kilele cha miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama
hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini
Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio
hilo.
Sehemu ya Umati wa Watu waliofika kwenye shamrashamra hizo leo.
Mwenyekiti
wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika jembe na
nyundo,ikiwa ni alama ya Mkulima na Mfanyakazi mara baada ya kuwasili
jioni ya leo kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya
kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya
Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
akishuhudia tukio hilo.
Mwenyekiti
wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za
kujiunga na chama cha CCM jioni ya leo.
Katibu
wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi
ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua
kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina
Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.
Mwenyekiti
wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi ya gitaa Msanii maarufu
wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awil,anaeshuhudia ni Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi.Zakia Meghji.
Wasanii
mahiri wa Filamu hapa nchini,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB
wakifuatilia yanayojiri hivi sasa ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine,mkoani Mbeya juu ya kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka
37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Mmoja
wasanii Mwimbaji na Mwigizaji wa filamu,ajulikanae kwa jina la kisani
kama Dokii akiimba mbele ya umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa CCM
waliofika kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa
chama cha CCM,ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya
Kikundi cha TOT Plus kiongozwa na gwiji wa mipasho hapa nchini,Khadija Kopa wakiimba jukwaani.
JB akizungumza machace kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutamka kuwa wamejiunga na chama cha CCM.
Wasanii hao wa Filamu wakifurahia jambo jukwaani.
Nape na wanachama wengine wakiserebuka kwa raha zao.
Mwenyekiti
wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Katibu
Mkuu wa chama hicho,Ndugu Kinana akiwapungia wananchi na wanachama wa
CCM,waliofika kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya
kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya
Sokoine,jijini Mbeya.
Nape Nnauye akiwa amembeba mtoto ambaye alionesha umahiri wake mkubwa wa kucheza ngoma ya kiasili.
Vijana wenye umri wa miaka 37 wakirusha njiwa angani kuashiria amani,utulivu na mshikamano wetu tulionayo.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye sherehe hizo jioni ya leo.
Mwenyekiti
wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akipiga gitaa kabla ya kumzawadia msanii wa
muziki maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awilo.
Vijana wa Halaiki.
0 comments:
Post a Comment