SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, November 29, 2011

Utajiri Wa Babu Loliondo Kufilisiwa

Mojawapo ya magari anayomiliki babu Ambilikile Masapile.
Na Mwandishi Wetu
Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’ (pichani), anaendelea kusakamwa na wagonjwa wanaodai hawakuponyeshwa na dawa yake, wapo walioweka nia ya kumburuza mahakamani lakini mpya ni pendekezo la kumfilisi.
Nyumba yake mpya.
Wanaharakati wameeleza kuwa miongoni mwa mashtaka ambayo wanamfungulia Babu Ambi, mojawapo ni kumfilisi mali zote alizochuma endapo atakutwa na hatia ya ulaghai, wakati wa kutangaza maono aliyopewa na Mungu kuhusu tiba ya kikombe.
Wanadai kuwa Babu Ambi, mkazi wa Kijiji cha Samunge, Loliondo, alitumia matatizo ya Watanzania  ya kuugua maradhi sugu ili kujinufaisha, hivyo akatengeneza ulaghai wa tiba ya kikombe kwa maelezo kwamba ni ufunuo aliopewa na Mungu.
Madai hayo yanakuja wakati ambao Babu Ambi ameukata, ameshakamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kisasa kijijini Samunge, pia anamiliki magari mawili ya bei mbaya, Toyota Land Cruiser (pick-up) na Isuzu (pick-up).
Babu Ambi, ameshahama nyumba chakavu aliyokuwa anaishi zamani na sasa anaendesha maisha yake kwenye mpya ya kisasa ambayo kwa Samunge, inaonekana ni kama Ikulu kwa jinsi inavyomeremeta.

Swaga Za Waheshimiwa John Mnyika na Joseph Mbilinyi aka Mr II Ndani ya Tamasha la Vinega

Mbunge wa Mbeya Mjini-Chadema Mheshimiwa  Joseph Mbilinyi aka Mr II akiwa jukwaani na Mbunge wa Ubungo-Chadema , John Mnyika. Wabunge takribani wanane walisindikiza uzinduzi wake huo ulioenda sambamba na uzinduzi wa kitabu kinachoeleza historia yake katika maendelea ya muziki wa Rap Bongo kwenye Tamasha lake lilofunika juzi Jijini Dar es Salaam Lilokwenda Kwa Jina laVinega
Mheshimiwa Mbunge Joseph akiwa anachana mistari jukwaani usiku wa kuamkia juzi, nyomi ilikuwa ya kutisha.

ULE WARAKA WA CHADEMA KWA RAIS JAKAYA KIKWETE JUU YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, 2011

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo toka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe baada ya kupokea  mapendekezo ya chama hicho juu ya kuundwa katiba mpya yatayozungumzwa kwenye mkutano huo wa kihistoria uliofanyika juzi Ikulu jijini Dar es salaam

Dk Asha -Rose Migiro:Wabunge Wekeni Mbele Maslahi ya Wananchi Mnaowawakilisha

Mhe.Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro akibadilishana mawazo na Waheshimiwa Wabunge John M. Cheyo na Betty Machunge wakati alipowakaribisha Ofisini kwake Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.Wabunge hao wapo hapa wakihudhuria mkutano wa wabunge ambao Naibu Katibu Mkuu aliufungua. Wabunge hao wanaliwakilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo.
Mhe. Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha-Rose Migiro akifungua mkutano wa siku mbili wa wabunge kutoka mabunge mbalimbali duniani mkutano huo unafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, kushoto kwake ni Rais wa Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, Bw. Nassir Abdulazizi Al-Nasser na kulia ni Katibu Mkuu wa IPU Bw. Anders B. Johson.

Monday, November 28, 2011

RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAHAFALI YA 11 YA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Jaji Mkuu Mh Mohamed Chande Othman mara baada ya kuwasili katika sherehe za mahafali ya 11 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, mkoani Tanga
 Rais Jakaya Kikwete akipokewa na Jaji Mkuu Mh Mohamed Chande Othman kwenye sherehe hizo
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Sheria mstaafu Mh Bakari Mwapachu
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Jaji Bwana
 Rais Kikwete akisalimiana na mwakilishi toka PPF
 Waalikwa wakimsubiri kumlaki mgeni rasmi
 Rais Kikwete akisalimiana na mke wa Jaji Mkuu, Mama Saada Othman

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MAKUBALIANO YA IKULU NA CHADEMA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe baada ya kupokea  mapendekezo ya chama hicho juu ya kuundwa katiba mpya yatayozungumzwa kwenye mkutano huo wa kihistoria uliofanyika jana Ikulu jijini Dar es salaam
 ----
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete na ujumbe wa serikali yake pamoja na viongozi wa Chama cha Demokrasia
naMaendeleo (CHADEMA), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho
MheshimiwaFreeman Mbowe leo, Jumatatu Novemba 28, 2011 wamemaliza mkutano wao wa siku mbili Jijini Dar es salaam kuhusu Muswada wa sheria ya mabadiliko ya
Katiba wa Mwaka 2011.

Mkutano huo uliofanyika Ikulu umefanyika katika mazingira ya maelewano

Pande mbili zimekubaliana kama ifuatavyo:-

1.       1.Pamoja na sheria hiyo kupitishwa na Bunge ipo haja ya kuendelea
kuiboresha ili ikidhi mahitaji na kujenga kuaminiana na muafaka wa
Kitafa.

2.      2. Kwamba yawepo mawasiliano na mashauriani ya mara kwa mara
kati ya serikali na wadau mbalimbali juu ya kuboresha sheria hiyo kwa lengo
la kudumisha muafaka wa Kitaifa kwenye Katiba Mpya.

Imesainiwa na;

 
Mhe. John John Mnyika
----------
 Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema.
Mhe. John Emmanuel Nchimbi
-------------

Waziri wa Habari, vijanaUtamaduni na Michezo

ZITTO KABWE: Kupandisha Posho Za Wabunge Ni Ukichaa Na Kutojali Hali Ya Nchi

Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.
Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.

Thursday, November 24, 2011

Makamu wa Kwanza wa Rais-Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Atembelea Baraza Za Mazungumzo Kwa Lengo La Kuwa Karibu Zaidi na Wananchi.

Maalim Seif akiwa katika barza ya kwanza ya mazungumzo Radio One Darajabovu jana. (Picha, Hassan Hamad.Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais-Zanzibar 
--

FILAMU YA C.P.U KUANZA KUONESHWA RASMI IJUMAA TAREHE 25 NOVEMBA 2011 MLIMANI CITY CINEMAX CENTURY

Evans Bukuku akitoa maelezo kuhusu filamu ya CPU ,Mkurugenzi wa Haakneel Godfery Mahendeka (Kushoto) na Director wa filamu iyo Karabani (Kulia).
Sauda Simba muhusika mkuu katika Filamu ya CPU.
  

Director wa Filamu ya CPU Karabani akitoa maelezo na Steven Sandhu muusika mkuu katika filamu ya CPU

Yemen Celebrates As President Steps Down

Yemen's authoritarian President Ali Abdullah Saleh agreed Nov. 23 to step down amid a fierce uprising to oust him after 33 years in power.
In this image made from video broadcast by Yemen State TV and accessed via APTN, Yemeni President Ali Abdullah Saleh signs a document agreeing to step down after a long-running uprising to oust him from 33 years in power in Riyad, Saudi Arabia, Wednesday, Nov. 23, 2011. 
Saleh, seated beside Saudi King Abdullah in the Saudi capital Riyadh, signed a U.S.-backed deal hammered out by his country's powerful Gulf Arab neighbors to transfer his power within 30 days to his vice president, Abed Rabbo Mansour Hadi.
In this April 15, 2011 file photo, Yemeni President Ali Abdullah Saleh waves to his supporters, not pictured, during a rally in Sanaa,Yemen after returned from medical treatment in Saudi Arabia. 
Saleh has signed an agreement to transfer power to his vice president. Saleh was shown on Arabic satellite television stations Wednesday Nov. 23, 2011signing a proposal by his country's powerful Gulf Arab neighbors to end his country's 9-month old uprising.
Yemeni female protestors march during a demonstration demanding the resignation of Yemen's President Ali Abdullah Saleh in Sanaa, Yemen, Monday, Nov. 21, 2011.
Arabic on the banner reads, "people are free, and they reject immunity and guarantee Saleh."

PICTURE OF THE DAY!!

The world's tallest Basketball player, British man Paul 'Tiny' Sturgess (L), measuring 
231.8cm high poses in front of the British inventor of the world's smallest legally roadworthy car Perry Watkins in his vehicle measuring 104.14cm high, 66.04cm wide and 132.08cm long at Guinness World Records Day in London on November 17, 2011.
Wacky Guinness world record holders got together to race their unlikely vehicles like the world's fastest toilet and smallest roadworthy car in London the mark the 7th annual 
Guinness World Records day.  
BEN STANSALL

Wednesday, November 23, 2011

Homa Ya Lowassa CCM Yapanda

• Mwenyewe adaiwa kujipanga kufichua siri NEC
na Mwandishi wetu
Jina la Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ndilo lililotawala mazungumzo miongoni mwa wajumbe vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Mbali ya kutawala mazungumzo, Lowassa amewagawa katika makundi mawili wajumbe wa vikao hivyo kwa kiwango ambacho baadhi ya wadadisi wa mambo wanakielezea kuwa ni cha hatari kubwa kwa ustawi wa chama hicho.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa kufanya mahojiano na watu mbalimbali unaonyesha kwamba ndani na nje ya vikao hivyo kumekuwa na harakati zinazoendeshwa na ama watu wanaomuunga mkono Lowassa au wale ambao wamejitoa mhanga kuhakikisha anaachia nafasi ya ujumbe wa NEC.

Hali hiyo ya mambo ilisababisha mara tu baada ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu (CC) jana watu wanaotaka kujua hatima ya mwanasiasa huyo ambaye alijiuzulu uwaziri mkuu Februari mwaka 2008 kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kikao hicho.

Wakati wajumbe wakiendelea na mkutano huo, habari ambazo chanzo chake hakijulikani zilisambazwa katika maeneo mbalimbali nchini na kisha zikachapwa katika mitandao ya kijamii zikieleza kwamba tayari CC ilikuwa imeshapendekeza kwa NEC uamuzi wa kuwavua uongozi Lowassa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.

Saturday, November 19, 2011

Saif Al-Islam Gaddafi Amepatikana

 Saif al-Islam Gaddafi
Serikali ya muda ya Libya inasema kuwa Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, amekamatwa.

Waziri wa Sheria wa serikali ya mpito, Mohammed al-Allagi, alisema kuwa Saif al-Islam amezuwiliwa karibu na mji wa Ubari, kwenye jangwa la kusini-magharibi mwa nchi.

Ripoti moja ilieleza kuwa hivi sasa amechukuliwa kwa helikopta kupelekwa Zintan, kaskazini mwa nchi.

Amekuwa akijificha tangu wapiganaji wa serikali ya mpito kuuteka mji mkuu, Tripoli, mwezi Agosti, na anasakwa na Mahakama ya Uhaini ya Kimataifa, kwa mashtaka ya uhalifu wa kivita.
Chanzo BBC SWAHILI.

RAIS KIKWETE ALIPOONGEA NA WAZEE JIJINI DAR JANA

 
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wazee katika mkutano huo jana.
 
Rais Jakaya Kikwete akiongoza viongozi wa mbalimbali na wazee wa Mkoa wa Dar es salaam kuimba wimbo mara baada ya kuongea na wazee wa jiji la Dar es salaam jana, kutoka kulia ni Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadick na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam John Guninita na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Dar es salaam Brigedia Mstaafu Hashim Mbita.
 
Wazee hawa wakiwa makini katika kusikiliza hotuba hiyo kutoka kwa Rais Dk Jakaya Kikwete jana.
 
Baadhi ya wazee walikuwa wakiandika baadhi ya mambo muhimu ambayo Mh. Rais Jakaya Kikwete alikuwa akiyazungumza jana.

Thursday, November 17, 2011

WADAU NAITAMBULISHA KWENU ISLAMIC SITE MY UMMAH FAIDIKA NA MASUALA MBALIMBALI YA DINI YA KIISLAMU KWA KUITEMBELEA JUMAA KARIM

ASALAM ALAIKUM WARAHMATULLAH WABARAKATHU, I HOPE YOUR DOING FINE.AND EVERYTHINGS GOING WELL. 
SHARE THIS LINK TO ALL MUSLIM AND INSHA ALLAH TABALAKAH WATAALAH ALLAH WILL REWARD YOU A GREAT REWARDS HERE IN THE WORLD AND HEREAFTER, AMIN.
"My Ummah" is a SITE created for the purpose of spreading the word of Allah to the Ummah(i.e Nations, Community), which was not only the main Sunnah of our beloved Prophet Muhammad (Pbuh) but of every Prophet sent by Allah (S.W) on the Earth to Mankind, which is now our responsibility to follow the same way Insha Allah.
Here you can listen QURAN, LECTURES FROM DIFFERENT SHEIKH, NASHEEDS, ONLINE RADIO, POETRY, WATCH DIFFERENT TV PROGRAMMES ABOUT ISLAM, ARTICLES and many more.
I HOPE YOU WILL BENEFIT FROM HERE AND SEND TO US YOUR SUGGESTION.
WABILAH TAWFIQ
THE LINK IS HERE BELOW:

Blatter Aadai "Hakuna" Ubaguzi Uwanjani

Rais wa Fifa Sepp Blatter ajichanganya kuhusu ubaguzi
Mlinzi wa England na Manchester United Rio Ferdinand amesema ameshangazwa na madai ya Sepp Blatter kwamba hakuna tatizo la ubaguzi katika mchezo wa kandanda uwanjani.

Syria Ina SikuTatu Kumaliza Ghasia

 SYRIA FLAG
Jumuiya ya nchi za kiarabu imeipa Syria siku tatu kumaliza mzozo unaoendelea nchini humo la sivyo itawekewa vikwazo vya kiuchumi.

Habari kutoka Damascus zinasema majeshi yalioasi yameendelea kulenga kambi za jeshi linalotii serikali.

Ni miezi minane ambapo waandamanaji wasiokuwa na silaha wamekuwa wakilengwa na wanajeshi watiifu kwa Rais Bashar Assad.

Hali imebadilika sasa na majeshi yalioasi yameanza kukabiliana na mahasimu wao.

Naye waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe anatarajiwa kufanya ziara maalum nchini Uturuki, kujadili hatua dhidi ya mzozo unaoendelea nchini Syria.

Duru zinasema kwamba majeshi yalioasi wanaojiita Jeshi Huru La Syria, yameshambulia vituo kadhaa vya kijeshi mjini Damascus na kuwaua wanajeshi kadhaa wa serikali ya Syria, hata hivyo madai hayo bado hayajathibitishwa.

Lakini ikiwa madai haya yana ukweli wowote, basi ni ishara kwamba huenda mzozo wa Syria umechukua mkondo hatari.

Jumuiya ya nchi za kiarabu imeonya kuiwekea Syria vikwazo vya kiuchumi ikiwa serikali ya Rais Assad haitakoma kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji na imetaka dhuluma hizo kukomeshwa katika kipindi cha siku tatu zijazo.

Ututruki pia inatathmini kuiwekea Syria vikwazo. Tayari Marekani na jumuiya ya Ulaya zimeweka vikwazo, japo haijabainika athari za vikwazo hivi ni zipi.

Nchi za magharibi zimeanza kutafakari mustakabali wa Syria bila uwongozi wa Bashar Al Asaad.

Hata hivyo pande zote ziko makini kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo.

Na BBC SWAHILI

KAMPUNI YA GURJAR YA INDIA YAMKABIDHI MH.MOHAMED DEWJI DOLA ELFU 15 KUMUUNGA MKONO KATIKA KULETA MAENDELEO JIMBONI KWAKE

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni za GURJAR GRAVURES  na GURJAR IMAGES PRIVATE LIMITED za nchini India Bw. Zainuddin Mahuwala (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Singida mjini Mh. Mohammed Dewji (katikati) hundi ya $ 15,000/= kwa ajili ya kusaidia jitihada zake za kuboresha Maendeleo katika jimbo lake la Singida Mjini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hizo Bw. Shubair Mahuwala.

Wednesday, November 16, 2011

Upuuzi Wa Masoud Kipanya Upo Mitaanii


Masoud Kipanya akiwa amepozi kwenye kaunda suti yake na si gwanda/vazi la CHADEMA.

UPUUZI WA MASOUD KIPANYA ni documentary ya dakika 47 ambayo nimeirekodi mwaka juzi katika mazingira ya kijiji kilichotumika kurekodia MAISHA PLUS.

Kutokana na Kulipuka Kwa Transifoma iliyopo Katika Kituo Cha Umeme cha Ubungo Jiji la Dar es Salaam na Visiwa Vya Zanzibar Vitakosa Umeme Kwa Siku Kadhaa

Moja ya Transifoma iliyopo katika Kituo cha Umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam(Ubungo Grid Sub Station) imeungua moto jioni hii.Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Naibu Mkurugenzi wa Tanesco, Bi. Sophia Mgonja amesema kuwa, kutokana na hitilafu hiyo Jiji la Dar es Salaam na Visiwa vya Zanzibar vitakosa umeme kwa siku kadhaa. Akifafanua zaidi juu ya tukio hilo, Mgonja alisema lilitokea baada ya kifaa cha kurekebisha nguvu ya umeme kiitwacho Reactor kuungua.Picha hizi zinawanyonyesha wafanyakazi wa kikosi cha zima moto wakizima moto katika Transifoma iliyokuwa ikiungua.
Picha kwa hisani ya Kulwa Mwaibale/GPL

African music celebrated at star-studded 2011 Channel O Music Video Awards

ON a night that a host of live performances celebrated African music at its most electric, young, gifted artists from Ghana, Nigeria, South Africa, Namibia, and Uganda were named winners at the 2011 Channel O Music Video Awards.

ZITTO KABWE AREJEA NCHINI KUTOKA INDIA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Mh. Zitto Kabwe.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Mh. Zitto Kabwe, aliyekuwa amelazwa hospitali nchini India kwa zaidi ya wiki tatu kwa matibabu, amerejea nchini baada ya kupata nafuu na anatarajiwa kuanza kuhudhuria vikao vya Bunge linaloendelea hivi sasa mjini Dodoma, kuanzia leo.

Tuesday, November 15, 2011

Muswada wa Katiba Mpya: Hotuba ya Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (Tundu Lissu)

Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mh. Tundu Lissu.

MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU (MB.)KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, 2011

(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007)

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,

Tarehe 11 Machi 2011, Serikali ilichapisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 katika Gazeti la Serikali la tarehe hiyo.

Muswada huo ulipelekwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Hati ya Dharura. Hata hivyo, baada ya upinzani mkubwa dhidi ya Muswada huo kujitokeza karibu nchi nzima, Bunge lililazimika kuondoa Hati ya Dharura na hivyo kufanya Muswada kushughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa kawaida wa kutunga sheria uliowekwa na kanuni za 80, 83 na 84 za Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano, 2007. Katika kufanya hivyo, Bunge – kwa kupitia Spika - liliiagiza Serikali kufanya mambo yafuatayo kwa mujibu wa Taarifa Rasmi ya Majadiliano Katika Bunge (Hansard) ya Kikao cha Nane cha Mkutano wa Tatu cha tarehe 15 Aprili 2011:

(a) “Muda zaidi utolewe kwa Kamati na wananchi kuufikiria Muswada huu. Katika kufanikisha hili, “... iandae Muswada huu kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi wenyewe waweze kusoma yaliyomo kwenye Muswada huo badala ya kupewa tafsiri tu na watu wengine;

(b) “Muswada uchapishwe kwenye magazeti na kutangazwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari ili kutoa fursa ya kutosha kwa wananchi wengi kuuelewa na kuutolea maoni;

(c) “Utangulizi wa Muswada huu uwekwe vizuri zaidi ili wananchi waelewe madhumuni ya Muswada huu, kwani imeonekana wazi wananchi wengi wanadhani tayari tumeanza kuandika Katiba, kumbe lengo la Muswada huu ni kutunga Sheria ya Kuunda Tume ya Kukusanya Maoni tu.” (uk. 31-32)

Mheshimiwa Spika,

WAANDISHI, POLISI WAJERUHIWA KATIKA VURUGU ZA WANANCHI MKOANI IRINGA JANA

Wananchi wakiishambulia nyumba yenye wanahabari, watuhumiwa na polisi kwa mawe.
Nguo za majeruhi ambaye alijeruhiwa kwa risasi baada ya kutaka kuwachoma moto wanahabari na polisi ndani ya nyumba hiyo.

Monday, November 14, 2011

Profesa Palamagamba Kabudi:ikumbukwe Kwamba Sote tutakufa Lakini Tanzania itabaki tuweka Maslahi Ya Taifa Mbele

 Waziri Mkuu na Mweneyekiti wa Semina Mhe. Mizengo Pinda akifungua semina ya mchakato wa marakebisho ya Katiba Mpya mjini Dodoma jumamosi
Spika wa Bunge Anne Makinda akifafanua jambo kwenye semina

Waziri Mohammed Aboud Mohammed:Jumla Ya Sh.Bilioni 1 na Millioni 100 Zimekusanywa na Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed
-- 
NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Jumla ya Shl.Bilioni 1 na Millioni 100 zimekusanywa na Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar hadi kufikia leo ikiwa ni michango mbalimbali kutoka kwa Taasisi,Watu binafsi na Wadau mbalimbali wa nje na ndani ya Zanzibar kutokana na ajali ya Meli ya Mv. Spice Islanders.
Hayo yameelezwa hivi leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed huko ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati alipokuwa akipokea Mchango wa Dola za Kimarekani 1444 sawa na Shl. Milioni 2 laki Moja na Hamsini na Nne na Mia Nane kutoka kwa Watafiti mbalimbali kutoka nje.