
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo toka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe baada ya kupokea mapendekezo ya chama hicho juu ya kuundwa katiba mpya yatayozungumzwa kwenye mkutano huo wa kihistoria uliofanyika juzi Ikulu jijini Dar es salaam
--
Mheshimiwa Rais,
Sisi ambao majina yetu yameambatanishwa chini ya Waraka huu tunakuandikia, kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kukushauri kutumia mamlaka yako chini ya ibara ya 97(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kukataa kuukubali Muswada waSheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 uliopitishwa na Bunge la
Jamhuri ya Muungano tarehe 18 Novemba, 2011. Sheria hiyo sasa inasubiri ridhaa yako Mheshimiwa Rais kabla ya kuanza kutumika.Ushauri wetuunatokana na imani yetu endapo Muswada huu utapata ridhaa yako na kuanza kutumika kama Sheria utakuwa na madhara makubwa kwa mchakato mzima wa utungaji wa Katiba Mpya na amani na utulivu wa nchi yetu kwa sababu zifuatazo zitokanazo na Muswada wenyewe.
USHIRIKISHWAJI HAFIFU WA WABUNGE NA WANANCHI
Mheshimiwa Rais, .
Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ulichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 11 Machi 2011.Muswada huo ulipelekwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Hati ya Dharura tarehe 9 Aprili 2011. Hata hivyo, baada ya upinzani mkubwa dhidi ya Muswada huo kujitokeza karibu nchi nzima, Bunge lililazimika kuondoa Hati ya Dharura na hivyo kufanya Muswada kushughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa kawaida wa kutunga sheria uliowekwa na Kanuni za Kudumu za Bunge.
Katika kufanya hivyo, Bunge liliiagiza Serikali kufanya mambo yafuatayo kwa mujibu wa Taarifa Rasmi ya Majadiliano Katika Bunge ya tarehe 15 Aprili 2011:Kusoma Zaidi Waraka Huu Bofya na Endelea.........>>>>>>>
0 comments:
Post a Comment