Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi ambaye ni Mwenyekiti wa kiduru wa Umoja wa Afrika AU amesema kuwa bara la Afrika linapaswa kupigania ruzuku za wakulima masikini ili bara hilo liwe na usalama wa chakula. Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa IMF zimezuia ruzuku za kilimo kwa wakulima masikini wa Kiafrika kutokana na gharama kubwa ya ruzuku hizo. Mutharika amesisitiza kwamba, nchi za Kiafrika zinapaswa kusimama kidete na kupigania ruzuku hizo za wakulima masikini, na kwamba uanachama mpya na jumuiya za utoaji misaada unapaswa kuwepo kwa kuzingatia uimarishaji ruzuku kwa wakulima wanaomiliki mashamba madogo hasa wanawake. Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika aidha ameongeza kuwa, haiyumkiniki wakulima wa Kiafrika kuweza kulima bila kupewa ruzuku, kwani ruzuku hiyo huelekezwa moja kwa moja katika ununuaji mbolea, mbegu, dawa za kuulia vijidudu, matrekta, vifaa vya umwagiliaji na huduma nyinginezo.
Friday, October 29, 2010
Mwenyekiti wa AU: Afrika inapaswa kupigania ruzuku za kilimo
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, October 29, 2010
Email This
BlogThis!
Share to Twitter
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment