Waziri mkuu mpya wa Japan Naoto
Kan ametangaza baraza lake lipya la mawaziri huku mwanasiasa mkuu wa
mrengo wa kushoto Yoshiko Noda akishikilia wadhifa wa waziri wa fedha
kama ilivyotarajiwa.
Viongozi wote hao wanaazimia kupunguza sehemu
kubwa ya deni la taifa hilo. Wadhifa zingine zilipewa mawaziri
waliokuwepo katika baraza la zamani. Bwana Kan alichukua wadhifa huo
baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri mkuu Yukio Hatoyama, kutokana na
mzozo juu ya kambi ya kijeshi ya Marekani katika kisiwa cha Okinawa.
Umaarufu wa chama tawala cha Democratic
ulididimia chini ya uongozi wa Hatoyama na wadadisi wanasema kuwa kuna
matumaini kiongozi huyo mpya atasaidia kukikomboa.
UN kuwekea Iran vikwazo vipya
Baraza la usalama la umoja wa
matiafa limeafikia azimio la kuiwekea Iran vikwazo vipya na linatarajiwa
kupigia kura azimio hilo hapo kesho.
Vikwazo hivyo vinalenga kudhibiti miradi ya
Nuclear ya Iran, na iwapo vitaidhinishwa basi vitaongeza ukaguzi wa
bidhaa zinazoingizwa nchini humo na kupunguza kuuziwa nchi hiyo silaha.
Mwandishi wa BBC katika umoja huo amesema kuwa
kuna baadhi ya nchi ambazo hazitarajiwi kupigia kura azimio hilo japo
hazina kura ya turufu.
Uturuki na Brazil wamesisitiza kuwa vikwazo
vipya kwa Iran vitahujumu uhusiano mwema katika eneo hilo na wamesema
kuwa kuna matumaini ya kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia kutokana na
makubaliano ya kubadilishana mafuta ya nuclear walioafikia hivi majuzi.
0 comments:
Post a Comment