Makamu wa rais wa Marekani Joe
Biden ameanza ziara ya siku mbili nchini Kenya.
Ziara hii imeanza kwa Bwana Biden kukutana
na Rais wa Kenya Mwai Kibaki katika ikulu ya rais mjini Nairobi.
Mazungumzo kati yao yanafanyika faraghani na baadaye viongozi hao
wanatarajiwa kuwahutubia waandishi wa habari.Biden anatarajiwa kufanya mazungumzo baadaye na Waziri Mkuu Raila Odinga, kabla ya kukutana na kamati ya bunge inayohusika na marekebisho ya kikatiba.
Makamu huyo wa Rais wa Marekani anatazamiwa kuwasilisha ujumbe wa Rais Barrack Obama kwa viongozi wa Kenya, swala muhimu likiwa marekebisho ya kisiasa, katiba na mageuzi mengine. Pia atazungumzia umuhimu wa usalama katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati hasa swala la Sudan Kusini na Somalia.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amealikwa mjini
Nairobi kukutana na kiongozi huyu wa Marekani. Baadaye Biden atasafiri
kuelekea Afrika Kusini kushiriki ufunguzi wa dimba la Kombe la Dunia
litakaloanza Ijumaa Juni 11.
BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment