SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, June 8, 2010

BREAKING NEWS: Mwanamuziki Oliver Ngoma afariki dunia

                      Mwanamuziki wa Gabon Oliver Ngoma
Mwanamuziki mashuhuri kutoka Gabon Oliver Ngoma ameaga dunia.
  Oliver aliyezaliwa Machi 23, 1959, alishamiri sana katika muziki ya Zouk na reggae, na alisifika sana pia kwa upigaji guitar.
  Aliingizwa katika fani ya muziki na babake ambaye pia alikuwa mwalimu wa ala mbali mbali za muziki. Oliver alijiunga na bandi ya shule Capo Sound alipokuwa akisomea taaluma ya uhasibu.Hata hivyo alionyesha ukaribu zaidi wa muziki na akapewa ufadhili wa masomo ya Uandishi na kupiga picha nchini Ufaransa.
  Ngoma, aliyepewa jina la Utani la Noli, alipata umaarufu zaidi kwa wimbo wake Bane, wa mwaka wa themanini na tisa uliochezwa katika nchi zote za Afrika na ngambo.

Unaweza kusikiliza wimbo wake Oliver Ngoma kupitia You tube:
http://www.youtube.com/watch?
BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment