Kutoka
kushoto ni muasisi wa chama cha watu wenye ulemavu waendesha Bajaj, Aly
Issa, Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ulemavu Taifa, John Paul na
Katibu Mkuu Muasisi wa Chama hicho, Juma Bilal.
Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
Na Denis Mtima/Gpl
CHAMA cha
watu wenye ulemavu nchini (CHAWATA) kimeiomba serikali iruhusu biashara
ya usafiri wa Bajaj mijini ifanywe na watu wenye ulemavu tu
Haya
yalisema leo jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa Chama cha Walemavu
nchini (CHAWATA) Bw. John Paul wakati akizungumza na wanahabari kuhusu
kuwajengea mazingira mema na rafiki walemavu katika matatizo
wanayoyapata katika usafiri na shughuli mbalimbali.
Mbali na
matatizo hayo, Paul alizungumzia pia kuwapatia walemavu elimu ya kutosha
ili kuepusha manyanyaso na kunyayapaliwa wanakofanyiwa katika jamii.
Akisisitiza
kuhusu walemavu kupewa biashara ya kusafirisha watu kwa Bajaji,
mwenyekiti huyo alisema hilo litawapunguzia matatizo walemavu ikiwa
watatengewa kufanya biashara hiyo ambayo hivi sasa hufanywa na watu
wengi ambao si walemavu.
Alisema kwa walemavu kufanya biashara hiyo, wataweza kujipatia vipato kwa ajili ya familia zao ambayo huwategemea.(
Alisema kwa walemavu kufanya biashara hiyo, wataweza kujipatia vipato kwa ajili ya familia zao ambayo huwategemea.(
0 comments:
Post a Comment