Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na Athumani Hamisi alipomtembelea nyumbani kwake Sinza Madukani jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ndugu Eric Shigongo akisalimiana na Athumani Hamisi alipomtembelea nyumbani kwake Sinza Madukani jijini Dar es Salaam, kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.Athumani Hamisi alikuwa Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Daily/Sunday News na Habari Leo, yanayomilikiwa na Serikali kupitia Shirika lake la Standard Newspaper, ambaye alipata ajali iliyomsababishia baadhi ya viungo vyake kutokufanyakazi.
Athumani Hamisi akizungumza machache juu ya hali yake inavyoendelea mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ndugu Eric Shigongo.(P.T)
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimjulia hali
Athumani Hamisi alipomtembelea nyumbani kwake Sinza Madukani jijini Dar
es Salaam, kushoto ni mtoto wake wa kwanza Msafiri Athumani na kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Glogal Publishers Ndugu Eric Shigongo.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza
waandishi wa habari ambapo alisema Serikali itaendelea kumsaidia
Athumani Hamisi na kutafuta suluhisho la kudumu.Athumani Hamisi alikuwa
Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Daily/Sunday News na Habari Leo,
yanayomilikiwa na Serikali kupitia Shirika lake la Standard Newspaper,
ambaye alipata ajali iliyomsababishia baadhi ya viungo vyake
kutokufanyakazi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Glogal Publishers Ndugu Eric Shigongo akiagana
na Mtoto wa kwanza wa Athumani Hamisi anayeitwa Msafiri Athumani.
Waziri wa
Habari utamaduni Sanaa na michezo Nape Nauye ameahidi kutatua
changamoto zinazomkabili aliyekuwa mpiga Picha na mwandishi mwandamizi
Athumani Hamis. Wazir Nape ametoa kauli hiyo alipomtembelea nyumbani
kwake , Sinza Dar es salaam akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Global Publisher Eric Shigongo.
Waziri
Nape ameamua kumtembelea Athmani kutokana na kutambua mchango wake
kwenye tasnia ya habari ambapo aliitumikia kwa muda mrefu kabla ya
kupata ulemavu. “Amefanya Kazi kubwa serikalini, sisi kama serikali
tunao wajibu wa kumsaidia”. “Nimechukua Yale yote ambayo yanachangamoto
kwake na tunachukua uamuzi wa kumsaidia,”alisema Wazir Nape.
Waziri
Nape amempongeza Rais MstaafuJakaya Kikwete kwa kumsaidia Athmani katika
kipindi chote cha uongozi wake na kwamba yeye kama Waziri mwenye
dhamana kwa kushirikiana na wadau wengine wataendelea kutoa msaada kwa
Athmani na familia yake.
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ndugu Eric Shigongo ametoa wito kwa Watanzania kutoa msaada kwa moyo mmoja.
0 comments:
Post a Comment