Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akipokewa kwa ngoma wakati alipokuwa anaingia Gangaramaya temple
inayotumiwa na watu wa madhehebu ya Budha nchini Sri lanka tarehe
16.11.2013.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akishangiliwa na watoto wadogo (chekechea) wa shule ya awali ya Carlton
iliyoko Colombo, nchini Sri lanka wakati Mama Salma na wake wa Marais na Wakuu
wa Nchi za Madola walipotembelea shule hiyo tarehe 16.11.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti
Dunya Liyanage, 8, anayesoma darasa la 3 katika Shule ya Msingi ya Meusnes
iliyoko mjini Colombo wakati Mama Salma na wake wa Marais kutoka nchi za madola
walipotembelea maonesho ya Kendraya tarehe 16.11.2013.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akifuatiwa na Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje wa India Mama Louise
Khurshid, na Mama Charlotte Scott, Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia wakipata
maelezo kuhusiana na Gangaramaya temple kutoka kwa Naibu Mkuu wa Temple hilo Van
Kirinda Assage tarehe 16.11.2013.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Kiongozi wa Gangaramaya Temple Van
Kirinda Assage.
Wake wa Marais na wakuu wa
nchi za Jumuia ya Madola wakimwangalia mama mmoja wa Sri lanka aliyekuwa
akitwanga kwenye kinu wakati walipotembelea maonesho ya Kendraya huko Colombo
tarehe 16.11.2013.
Mama Salma Kikwete akiwa
pamoja na wake wa Marais kutoka nchi za Jumuia ya Madola wakiangalia jinsi
mwanaume na mwamamke wakishirikiana kufinyanga vyungu
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Sri lanka
Madame Shiranthi Rajapakse ambaya pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa Shule za
Carlton nchini humo wakati walipokutana kwenye moja ya shule hizo iliyoko
Colombo tarehe 16.11.2013.
Picha na John Lukuwi
0 comments:
Post a Comment