SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, January 1, 2015

SHEREHE YA ‘ESCROW’ NOMA, WATOTO WA KIGOGO WAFANYA BETHIDEI YA MAMILIONI

Bethidei ya Hassan na Khadija Dilunga wakiwa na makapu ya fedha.


Stori: Hamida Hassan
WAKATI dunia ikiingia Mwaka Mpya wa 2015, taarifa ikufikie kwamba kigogo mmoja ambaye ni mfanyabiashara maarufu jijini Dar amewaangushia wanaye, Hassan na Khadija Dilunga sherehe ya kuzaliwa ambayo imepachikwa jina la ‘Escrow’ kufuatia kufuru ya fedha iliyooneshwa na wahusika hivyo kuwa ndiyo gumzo la mjini kwa wikiendi iliyopita.

MSHANGAO!
Sherehe hiyo ilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Msasani Tower jijini Dar juzi ambapo waalikwa wengi walijikuta wakibaki midomo wazi kwa vile wakati wanafika nje walijua ni harusi ya mtoto wa mtu mzito serikalini lakini walipozama ndani walipigwa butwaa kukuta ni ‘bethidei’.
“Du! Ni sherehe ya aina yake, watoto wameingia kama maharusi kwa kumwagiwa maua tena wana ‘meidsi’ na upambaji wa ukumbi unatisha,  naona umesheheni mapambo ya gharama kubwa,” alisikika akisema mwalikwa mmoja huku akiendelea kushangaa maandalizi hayo ya kukata na mundu kama si shoka!
KULA, KUNYWA ZAIDI YA HARUSINI
Taarifa zaidi zinasema kuwa, waalikwa walikula vyakula vya kila aina tena vya gharama. Walikunywa mvinyo wa bei mbaya na vitu vilikuwa vya kumwaga kuliko hata inavyokuwa harusini.”
Keki za kifahari na shampeni kibao.

WABADILI NGUO UKUMBINI
Kama vile haitoshi, watoto hao wakiwa ukumbini hapo huku wakikata keki kubwa na kulisha wazazi na wageni waalikwa, kuna wakati walikwenda kubadilisha nguo ambapo kama mwalikwa aliwaona wakati wanaingia, ilikuwa tofauti na wakati wa kutoka. Hassan kwa juu alivaa T-shirt iliyoandikwa Air Jordan ambapo ilikuwa sare na ya baba yake aliyevaa naye Air Jordan.
JEURI YA FEDHA
Lilipowadia suala la kutuza sasa, watoto hao walimwagiwa mifedha hasa noti nyekundu (msimbazi) na madolari (dola) hadi wakajaza vikapu viwili walivyovishika mapajani. Hata hivyo, haikujulikana kiasi cha pesa kilichopatikana!
ZAMU YA MAMA WATOTO SASA
Mama huyo wa watoto hao (Tunt) naye ilipofika zamu yake ya kutoa zawadi, aliwapa simu aina ya Sumsung Galax note 3 na mikufu ya dhahabu ambayo kwa mwonekano ni kuanzia gramu tano na kuendelea.
Waalikwa wakifungasha fedha ukumbini.
FUKO LA FEDHA
Katika hali ya kushangaza, mama huyo alijaza fedha kwenye FUKO LA RAMBO na kuondoka nalo, utadhani ilivyokuwa kwa waliochota fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow ambayo kwa sasa ni gumzo nchini kote.
“Jamani naona leo hapa ni kama Escrow kwa kwenda mbele. Hebu angalia ule mfuko ya rambo, umejaa fedha. Sijui ndiyo mifuko aina ya sandalusi aliyoisema Zitto Kabwe? (mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali).
Mmoja wa waalikwa akiwa na rambo la fedha.
RASHIDA WANJARA NDANI
Katika sherehe hiyo iliyokuwa na watoto wengi wa mjini, staa pekee aliyeshaini ni aliyekuwa Miss Mara 2000/01,  Rashida Wanjara ambaye alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.
HAIJAWAHI KUTOKEA
Akizungumzia shughuli hiyo, Wanjara alisema kwamba haijawahi kutokea sherehe ya kuzaliwa kuwa vile na kutikisa jijini Dar kwani watu walikula na kujiachia na kilichotikisa zaidi ni fedha zilizomwagwa ukumbini hapo.
“Kiukweli mihela ilinifanya nishangae kwani mama shughuli aliondoka na mfuko wa rambo wa fedha ambao uliwashangaza watu wengi ni kwa jinsi alivyotunzwa, lakini pia kuna marafiki wa mama shughuli nao niliwaona wakibeba fuko la fedha kichwani,” alisema Rashida.
Waalikwa wakigonga chiazi.
MASWALI YA WAALIKWA
Baadhi ya waalikwa wa shughuli hiyo walikuwa wakiulizana kuwa, kama sherehe ya kuzaliwa kwa watoto ‘kufuru’ inakuwa vile, je kwenye harusi itakuwa vipi?!“Sasa jamani, hii bethidei ndiyo makamuzi yote haya, msosi, vinywaji, mafwedha. Je, siku ya harusi ya mtoto mmoja kati yao itakuwaje?” alihoji mwalikwa mmoja bila kujua paparazi alikuwa jirani yake.
BENDI YA TAARABU YAHUSIKA
Kwa upande wa burudani, Bendi ya Taarab ya Ustadhi ilihusika ambapo ilitumbuiza na kukonga vilivyo nyoyo za wageni waalikwa ambao waliondoka ukumbini hapo wakiwa vizuri. Picha ni kwa msaada wa Mashughuli Blog.

CHANZO: BOFYA HAPA

0 comments:

Post a Comment