SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, January 1, 2015

Mwaka Mpya: Maafa China 35 wafariki

Umatti wa watu waliokanyagana na wengine kufa nchini China wakati wakiupokea mwaka mpya 2015
Sherehe za kuupokea mwaka mpya 2015 zimeguka kuwa majonzi baada ya watu thelathini na watano kufa kwenye taharuki ya kukanyagana kwenye msongamano wakati wakiiupokea mwaka mpya.
Maafa hayo yametokea katika mji Shanghai ambapo maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika ili kuupokea mwaka mpya.
Chanzo cha taharuki hiyo bado haijafamika lakini vyombo vya habari vya nchi hiyo vimenukuliwa vikisema imetokana na maelfu ya watu kuzuiwa kugombea fedha bandia zilizotupwa eneo hilo kutoka katika jengo moja.
Chanzo: Bbc Swahili

0 comments:

Post a Comment