Ni
kama juzi tu tuliposhangilia kuanza kwa mwaka mpya 2014. Wakati mwaka
huu unaanza ulikuwa na shauku kubwa, ulijipangia mipango mikubwa na
ulisema 'mwaka huu 2014 ni mwaka wangu'. Ikaisha Januari na kuanza
Februari ilipofika Mei hukuwa na kumbukumbu yoyote kuhusu mambo yale
uliyojiahidi wakati ukisherekea mwaka mpya. Na sasa mwaka umeisha tena,
umeanza mwaka 2015, utajiwekea malengo makubwa na kusema huo ni mwaka
wako!Umekuwa
unarudia utaratibu huu kila mwaka na bado hujastuka muda ambao
unapoteza kadiri miaka inavyozidi kwenda. Leo nataka kwa pamoja tuende
hatua kwa hatua jinsi ambavyo unaweza kuutumia vizuri mwaka huu 2015.
Tunachokwenda kujadili hapa kitakuhitaji wewe kuwa makini na kukifanya
ili uweze kubadili maisha yako. Unapoanza
mwaka 2015, tenga muda usiopungua saa moja. Katika muda huo kaa sehemu
ambayo ni tulivu na hutopata usumbufu wowote. Zima simu yako/zako na
kukaa wewe kama wewe. Katika muda huo sahau kuhusu matatizo
yanayoendelea kwenye maisha yako, sahau kuhusu watu wanaokudai au
unaowadai na hapa baki na nafsi yako tu. Katika muda huu kuwa na kitabu
chako cha kuandika mipango yako na kalamu. Utakachokifanya hapa ni wewe
kutafakari maisha yako yalipotoka, yalipo sasa na yanakoelekea.Umetoka wapi?Katika
ukurasa mmoja wa kitabu chako andika kichwa cha habari, 'nimetoka
wapi?' Katika ukurasa huu andika mambo yote yaliyotokea kwenye maisha
yako kwa siku za nyuma. Andika ndoto zako zote ulizokuwa nazo tangu
ukiwa mtoto, ukiwa shuleni na hata ulipokuwa unaanza kufanya kazi.
Andika ni jinsi gani ulikuwa unafikiria maisha yako yatakuwa baada ya
kipindi fulani. Pia tumia nafasi hii kuandika matukio makubwa
yaliyotokea kwenye maisha yako na ambayo yamebadili sana maisha yako. Katika
sehemu hii andika maamuzi ambayo umewahi kufanya kwenye maisha yako na
yakakuletea mafanikio makubwa. Na pia andika maamuzi ambayo umewahi
kufanya na ukawa umekosea sana, yaani yakakufanya upoteze au uingie
kwenye matatizo. Wakati unaandika mambo haya usitoe hukumu yoyote, yaandike kama yalivyo na baadae utajua ni jinsi gani ya kutumia mambo haya. Uko wapi sasa?Baada
ya kuandika ni wapi ulipotoka, fungua ukurasa mwingine na juu andika
'nilipo sasa'. Katika ukurasa huu andika mambo yanayoendelea sasa kwenye
maisha yako. Andika ni kazi au biashara gani unafanya. Andika ni
familia gani unaishi nayo. Andika ni kipato gani unapata sasa na pia
andika changamoto gani unazopitia sasa. Andika
ni hofu gani unaipata kila siku na inatokana na nini. Andika pia kama
kazi au biashara unayofanya unaipenda au inakusukuma kufanya makubwa
zaidi kwenye maisha yako. Ninaposema
andika, namaanisha utafakari kisha uandike kile ulichotafakari. Pia
kuwa mwaminifu sana na zoezi hili, usijaribu kujidanganya mwenyewe.
Hakuna yeyote atakayeona ulichoandika hivyo andika ukweli wako wote. Unaelekea wapi?Hii
ni hatua ya mwisho ya kuyaelewa maisha yako ili uweze kuchukua hatua
sahihi. Katika hatua hii fungua ukurasa mwingine kwenye kitabu chako na
kisha andika ninaelekea wapi? Katika ukurasa huu andika vitu vyote
ambavyo unataka vitokee kwenye maisha yako. Andika ni kazi gani unataka
kufanya na katika ngazi gani, kama ni biashara andika ni biashara gani
unataka kufanya na unataka kuifanya kwa kiwango gani. Andika ni jinsi
gani unayaona maisha yako miaka mitano ijayo, kumi ijayo na hata
ishirini ijayo? Jiulize
kama ungepata nafasi ya kubadili maisha yako, ni maeneo gani hasa
ambayo ungeyabadili. Jiulize kama ungejua kwamba huwezi kushindwa ni
kitu gani ambacho ungekifanya? Na pia jiulize kama fedha isingekuwa
tatizo kwako ni kazi au biashara gani ambayo ungeifanya? Tafakari
kwa kina kuhusu maisha yako na unataka yaelekee wapi. Andika chochote
ambacho unafikiria au unataka kitokee kwenye maisha yako. Mpango mkakatiBaada ya kujua umetoka wapi, uko wapi na unaelekea wapi sasa ni muda wa kuja na mpango mkakati wa maisha yako.Kwa
kuangalia ulipotoka angalia ni makosa gani uliyofanya na kisha jifunze
kutokana na makosa hayo. Baada ya kujua ni kipi umejifunza usiendelee
kurudia rudia tena makosa hayo. Pia angalia ni mambo gani uliyofanya
yakakuletea mafanikio na angalia ni jinsi gani unaweza kufanya tena ili
kupata matokeo bora zaidi. Kwa
kuangalia ulipo amua kwamba hutaendelea kama ulivyo sasa. Tambua kwamba
unahitaji kufanya mabadiliko ili maisha yako yaweze kuwa bora zaidi.
Angalia ni mambo gani unayofanya ambayo yanakupotezea muda na
hayakusaidii kufikia malengo yako kwenye maisha.Baada
ya kuangalia sehemu hizi mbili, ulipotoka na ulipo sasa ni muda wa wewe
kupanga vizuri kule unakotaka kufika. Kwa kuwa umeshajua ni wapi
unataka kufika na ni jinsi gani unataka maisha yako yawe, sasa weka
malengo yako. Unapoweka malengo weka ya muda mfupi na ya muda mrefu. Na
pia weka mipango ya kutekeleza malengo hayo. Mambo muhimu ya kuzingatia wakati unaweka malengo yako Jinsi
unavyoweka malengo ina athari kwenye kufikia malengo yako. Kama utaweka
tu malengo kwa sababu kila mtu anasema mwaka huu nafanya hiki au kile
basi utajikuta unashindwa kufikia malengo hayo. Yafuatayo ni mambo
muhimu unayotakiwa kuzingatia wakati unaweka malengo yako; 1. Andika malengo yakoMoja
ya kosa ambalo watu wengi huwa wanafanya wakati wa kuweka malengo ni
kusema tu na kuishia hapo. Unatakiwa uandike malengo yako ili kuweka
msisitizo zaidi. Unapoandika malengo yako inakufanya ufikiri zaidi na
hivyo kuyapa uzito. Ila ukisema tu nataka kuwa na biashara kubwa na
kuishia hapo hakuna chochote kitakachokusukuma kufikia lengo hilo. 2. Andika malengo kwenye maeneo yote muhimu kwenye maisha yakoMara
nyingi watu wanaposikia kuweka malengo wanafikiri unaweka malengo ya
kazi, fedha au biashara. Kila eneo la maisha yako linatakiwa kuwekewa
malengo. Hivyo unahitaji kuweka malengo ya kazi au biashara, weka
malengo ya fedha, weka malengo ya mahusiano, weka malengo binafsi na pia
weka maelengo ya kiafya. Ili kuwa na maisha yenye mlinganyo unahitaji
kuwa na malengo katika maeneo haya muhimu kwenye maisha yako. 3. Weka utaratibu wa kupima malengo yakoBaada
ya kuweka malengo na mipango ya maisha yako ya baadae ni muhimu kuwa na
utaratibu wa kuweza kupima malengo yako. Ni muhimu uweze kupima kama
upo kwenye njia sahihi ya kukufikisha kwenye malengo yako au umeshapotea
njia. Ukikosa utaratibu wa kujipima utakuja kustuka mwaka mwingine
umeisha na hujafanya jambo lolote la maana. Ni
muhimu sana kwako kufanya zoezi hili la kutathmini maisha yako. Unaweza
kuona huwezi kupoteza muda kufanya haya tuliyojadili hapa, ila
unapoteza muda mwingi sana kwa kufanya mambo ambayo hujui kama
yanakufikisha kwenye malengo yako maishani. Muda unaotumia kupanga
unaokoa muda ambao ungepoteza kwa kufanya jambo bila ya kupanga.
Umemaliza mwaka 2014 kwa kujua ni wapi ulipokosea na wapi ulipofanya
vizuri katika miaka yote iliyopita na anza mwaka 2015 ukiwa na mtazamo
mpya wa kuleta mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako.
Cha kujiuliza kikubwa,je hayo maisha unayoishi leo ndiyo ilikuwa ndoto yako ??Mfano
sasa hivi kuna mbinu nyingi za kufanya ili ubadili maisha
yako...jiulize kama kuna walionza kwa kufanya biashara na Forever Living
na mtaji wa 375,000/= na leo wanaingiza zaidi ya Tsh milioni 15 kila
mmoja na wanamiliki magari ya kifahari,mapya na ya kisasa kama Ford
Ranger,Land Rover Discovery4,Jeep Cherokee (U.S)Edition ya 2013,kwa nini
wewe usifanye??Na unaposema biashara hii hauwezi,je hyo unayoiweza
imekufanyia nini?kumbuka mwaka 2015 uwe karibu sana na watu
waliofanikiwa,hao watakuongezea chachu ya kufikia ndoto zako...ila
ukikaa karibu na walioshindwa hao watakusaidia kuangamiza ndoto
zako..kumbuka mafanikio au kushindwa kwako kupo mikononi mwako na
hulazimishwi...Chukua Hatua, Kama umefurahishwa na ujumbe huu,Tupigie
simu +255 783 149 561 Tukushauri cha kufanya,..ni bure.. Tunakutakia Heri Ya Mwaka Mpya 2015 Wenye Mafanikio Tele!
0 comments:
Post a Comment