
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye
koti la suti) akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili
kuhuduria sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni,
Kusini Pemba na kupokelewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na
Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
Bw. Al Amin Yusuph (kulia) aliyeambatana na Mshauri na Mkufunzi kutoka
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi.
Rose Haji Mwalimu (aliyeongoza mbele).
Na Mwandishi wetu, Pemba
SERIKALI
ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba itaendelea kuruhusu kuanzishwa kwa
Redio za jamii kutokana na umuhimu wake katika kuhimiza maendeleo na
kutumika kama daraja kati ya wananchi na serikali yao.
Hayo
yalisemwa na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na
watoto, Zainab Omar Mohammed wakati akizundua kituo cha redio ya jamii
jimbo la Mkanyageni, Mkoani Pemba.
Shughuli
hiyo ambayo ilifanyika kama sehemu ya shamra shamra za sherehe za
mapinduzi kutimiza miaka 51 zilihudhuriwa pia na wafadhili wa mradi huo
ambao ni Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO).
Waziri
huyo alisema kwamba uzinduzi wa kituo cha redio ya jamii katika jimbo
la Mkanyageni Mkoani Pemba ni moja ya azma ya serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kuwapa haki wananchi wake ya kupata habari ikiwa ni sehemu
muhimu sana ya maisha ya wanadamu.

Munekano wa sehemu ya jengo la Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba kabla ya kuzinduliwa rasmi.
Alisema
habari ni kitu muhimu sana katika maisha ya sasa na wakati taifa
likiadhimisha miaka 51 ya mapinduzi yaliyolenga kubadili maisha ya
wazanzibari uwapo wa redio za jamii ni kitu ambacho kitasukuma mbele
zaidi madhumuni ya mapinduzi , kumkomboa mzanzibari kiuchumi na
kifikira.
“Redio
hizi Jamii, zimewekwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
madhumuni ya kuwapa fursa wananchi kupata habari,kupata burudani, kupata
elimu, lakini pia kutoa fursa ya kutoa mawazo yao kupitia redio hizi
ili serikali ipate kujua zaidi nini hasa changamoto za wananchi na iweze
kuzifanyia kazi kwa urahisi zaidi” alisema Waziri Zainab.
Pamoja
na kuushukuru Umoja wa mataifa kwa kusaidia redio za jamii aliutaka
Umoja huo uendelee kuimarisha uwezo wa redio hizo ili wananchi wazitumie
kupata maendeleo.
Naye
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amesema
Umoja wa mataifa unajisikia fahari kuwezesha asilimia 60 ya wazanzibari
kusikiliza redio za jamii na kuzitumia katika maendeleo yao.

Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
aliyeambatana na mkewe akisalimiana na Ofisa mdhani kutoka Wizara ya
Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya
usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed mara baada ya kuwasili eneo
la tukio.
Alisema
umoja huo utaendelea na ushirikiano wake na serikali ya Mapinduzi
Zanzibar ya kuweka mazingira ya upatikanaji wa habari kuwa bora zaidi,
ushirikiano ambao waliuanza mwaka 2008 wakati wa kutengeneza sera ya
utangazaji.
Alisema ni sera hiyo iliyowezesha kuwepo kwa redio za jamii na utangazaji wa umma.
Alisema
Redio za jamii ni msaada mkubwa katika kutoa elimu kwa jamii
inayozunguka kituo hicho na kusema kwamba ni imani yake kituo cha Mkoani
kitafanya kazi iliyokusudiwa kwa kuhamasisha mawazo chanya ya maendeleo
na kuleta ushirikiano na amani inayotakiwa katika jamii.

Amesema Umoja wa Mataifa umewezesha kituo hicho vifaa vya utangazaji na kutengeneza uwezo wa wafanyakazi wa chombo hicho.
Amesema
kupitia mradi wa uwezeshaji demokrasia (EDP) unaoendeshwa kwa pamoja na
UNESCO na UNDP chini ya makubaliano ya msaada kwa serikali ya Tanzania
na Umoja wa Mataifa (UNDAP) , Umoja wa Mataifa umetoa mtambo wa kurushia
matangazo wenye nguvu za Watts 600 unaoweza kusambaza matangazo yake
eneo lote la Kusini pemba.
Pamoja na mtambo huo na vifaa vingine vya studio vilitolewa na
kumefanyika ufundishaji wa watangazaji namna bora ya mawasiliano na
menejimenti ya habari na utawala.
Mratibu
huyo aliitaka serikali na taasisi zake kukitumia vyema kituo hicho
katika kuhakikisha kwamba maendeleo yaliyokusudiwa kwa jamii
yanapatikana kupitia vipindi mbalimbali vya kuelimishana.

Pia
aliwataka waendeshaji wa kituo hicho kuwa makini na kuwajibika kwa umma,
kauli ambayo awali pia ilielezwa na Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya
habari Utamaduni , Utalii na Michezo Juma Yakufi aliyetaka sheria na
taratibu za mawasiliano kuzingatiwa.
Alitaka
vipindi vitakavyotengenezwa kuzingatia utu, silka na utamaduni wa
Mzanzibari na redio hiyo kuendeshwa kwa mujibu wa masharti ya redio
jamii kwa kuhakikisha hawaingiliwi na taasisi yoyote na kuendeshwa kwa
manufaa ya jamii na sio manufaa ya mtu mmoja mmoja.
Naye
Mwa redio hiyo Ali Abbas pamoja na kushukuru kusaidia kuanzishwa kwa
redio hiyo aliitaka jamii kuitumia vyema nafasi waliyopewa kuendeleza
mbele maendeleo yao na kutumia upashanaji habari kutanzua changamoto za
maendeleo.




















Mgeni
rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na
watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed katika picha ya pamoja na wajumbe wa
bodi ya Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba.
Mshauri
na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akiwa kwenye picha na wanafunzi
wake wa vituo vya redio jamii ya Mkoani na Micheweni mara baada ya
sherehe za uzinduzi.
Kikundi
cha Ngoma ya Msembwe cha kisiwani Pemba kikitoa burudani kwenye
uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani uliofanyika mwishoni mwa juma Kusini
Pemba.
0 comments:
Post a Comment