"NAMSHUKURU MUNGU KWA KUCHAGULIWA KUSHIRIKI KAMA MSIMAMIZI KWENYE WORLD CUP YA WAPISHI INAYOFANYIKA KILA BAADA YA MIAKA 4 NITAPEPERUSHA BENDERA YA NCHI YANGU TANZANIA NI JAMBO LA KUJIVUNIA SANA".
Mpaka sasa Chef Issa Kapande mbali ya kushinda tuzo nyingi tofauti ndani na nje ya nchi katika fani yake ya upishi pia anashikilia rekodi ya kua Chef Mtanzania Msomi na mdogo kuliko wote aliewahi kufungua na kuongoza hotel ya nyota tano ( Certified Executive Chef) akiwa na umri wa miaka 25 tu. Hili ni jambo la kujivunia sana.
Mola ajaliapo anatamani sana mwaka 2018 aipeleke Tanzanian chefs national team kwenye mashindano haya na anaimani atafanya vizuri tu kwani kuna wapishi wazuri sana nyumbani Tanzania ingawa wamekosa nafasi au muongozo wa kuweza kuonyesha uwezo wao Mungu ibariki Tanzania.
Chef Issa Akiwa na Mr Wyne aliekua FB manager wakati huo.
Tuzo ya heshima kwa kutambua mchango wa chef Issa kwa chakula cha kiafrica ndio tuzo ya mwisho aliopata mwaka jana mwezi wa 10
Chef issa akiwa na jaji mkuu wa mashindano ya kumpata mpishi bora wa mwaka wa Sweden.
Chef Issa Akiwa kazini anamuwekea kuku wa kuoka viungo tayari kwa kuliwa.
Hapa chef Issa Kapande akiwa na management team ya East African All suits hotel alipofungua hotel ya nyota tano na kuandika historia ya kua certified Tanzanian Executive chef katika umri wa miaka 25 tu. Hotel ilifunguliwa na aliekua Makamu wa Rais wakati huo ambaye sasa ni Rais wa Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati walioketi).
kwa habari zaidi za kombe la dunia la wapishi unaweza zipata hapa http://www.vatel.lu/competitions.php
kwa habari zaidi za mapishi na za chef Issa unaweza like facebook pagehttps://www.facebook.com/pages/Active-chef/509561519067534
0 comments:
Post a Comment