Labda hapa niwaeleze huenezwa na nini?
Ugonjwa huu huenezwa na Mbu aina ya aedes mosquito, na hawa mbu wamegawanyika makundi 2 hivi, nafikiri watu wa taxonomy wataweza kunisaidia vizuri zaid, na specifically mbu hawa hubeba vijidudu viitwavyo dengue virus. Vijidudu hivi huwa na selflimiting kama walivyo virus wengine hivyo jinsi ya kupona hakuna dawa maalum.
Dalili za ugonjwa huu
Dalili huanza kuonekana siku 4-7 baada ya kuumwa na mbu mwenye hawa virus.Dalili za dengue ya kawaida
homa kali zaid ya 40 degrees
maumivu makali ya kichwa na hasa kipanda uso
maumivu ya viungo na misuli
harara mwili mzima ambazo hutokea baada ya siku 3-4 baada ya kuumwa na mbu
Pia Dengue hemorrhagic fever huwa ni pronounced zaid na hii huweza kusababisha kifo.
dalili zake ni
kutokwa na damu puani, kwenye fizi ama kutoka bruises zenye rangi ya wekundu kwa mbali kwenye ngozi
Dengue shock syndrome ni severe form na hii hutokea kwa watoto ambao wamekuwa re- infected na huyu mbu na mara yingi sana husababisha mauti kwa watoto hawa. dalili zake huwa ni
kutokwa damu kwa wingi massive bleeding
shock (very low blood pressure)
TIBA:
HAKUNA TIBA MAALUM AMA KAMILI KWENYE HUU UGONJWA KAMA ILIVYO KWA BAADHI YA MAGONJWA YASABABISHWAYO NA VIRUSI.
=========
Lakini mgonjwa anatakiwa apate muda wa kupumzika, anywe fluids kwa wingi na ameze dawa za kushusha homa hasa paracetamol. Asprin haziruhusiwi kabisa kutumiwa unapoona dalili hizi sababu nitazieleza baadae.
kwa mgonjwa ambaye na shock yani kutetemeka ama yuko na hali mbaya sana basi ni bora awah hospitali na hapo atapatiwa matibabu ya haraka na kumwongezea electrolytes ili kuokoa maisha ya mgonjwa.
HOMA YA DENGUE NI NINI?
Homa ya Dengue ni ugonjwa unaoenezwa kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes mwenye virus vya ugonjwa huu. Mbu hupata virusi vya homa ya Dengue anapomuuma mtu mwenye ugonjwa huu.
Ugonjwa huu unaenezwa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kwa kuumwa na mbu huyu.
DALILI:
Homa kali ya ghafla
Kuumwa kichwa hususani sehemu za machoni
Maumivu makali ya viungo na misuli ya mwili
Kichefuchefu au kutapika
Kutokwa na damu kwenye fizi, na sehemu za uwazi za mwili.
Uchovu
ukimsikia ndugu au jamaa yako anasema kuwa na dalili hizi muwahishe hospitali mapema.
SAMBAZA KUWASAIDIA NA WENGINE.