Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Keysha, akiwa na mtoto wake wa kiume aliyejifungua salama, ambaye anaongeza idadi ya watoto wake na kuwa wa pili. Keysha amejifungua mtoto huyo juzi jumatatu katika Hospitali ya Mount Mkombozi, iliyopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Pichani ni rafiki zake waliofika hospitalini hapo kumjulia hali, hongera Keysha.