Taarifa ya kushambuliwa na mkurugenzi wa halmashauri na mkiti wa halmashauri
Ndugu zangu wana babati
Leo kulikuwa na Kikao cha kawaida cha mipango miji miongoni mwa mambo tuliyojadili ni orodha ya majina ya wananchi waliolipia mashamba Kule shamba la katanini, wakati wakikao hoja ilitolewa namkurugenzi anayekaimu, Kuwa orodha hiyo imechakachuliwa , Kikao kikaazimia kuwa tuletewe orodha iliyotolewa wizarani, chakushangaza mwenyekiti wa halmashauri bw Fara akajenga hoja Kuwa orodha hiyo ibaki halmashauri Kuwa Siri, na madiwani wote wa CCM waliafiki hivyo, nami nikajenga hoja kwa mujibu kanuni Kuwa kila Mjumbe kwa mujibu wa kanuni anatakiwa Kuwa na orodha hiyo.

ndipo nilipowashinda kwa hoja japo niko pekeyangu Kama
Diwani na mbunge wa chadema , Kikao kikaendelea hadi mwisho , Kikao
kilifungu mida ya saa Tisa kasoro, alasiri , Kikao Kilivyo ahirishwa
mkurugenzi wa mji akanisogelea na kunitaka nimkabidhi kabrasha langu,
ndipo akaninyanganya kwa Nguvu kabrasha nililonalo mikononi akidhani
orodha ile ya majina ya wananchi iPo hapo kumbe ilikuwa Kwenye pochi
yangu alipogundua si yo,akanirudia wakati Huo mkiti wa halmashauri
aliyeondoka Kikao Kilivyoahirishwa akasikia kuna Kelele akarudi ukumbi
,ndipo alipomwamuru mwandishi wa vikao Vya halmashauri Bw Mangalili
afunge mlango Nayeli akafanya hivyo, a kawa M/Kiti wa halmashauri bw
Fara akisaidiana na mkurugenzi wakanikaba Kabbali , wakanichana blauzi
yangu Kama inavyoonekana Kwenye picha ,nakukwapua pochi yangu Mithili ya
wezi au vibaka wakasachi hiyo orodha ya majina ya wananchi na vitu
vingine na fedha ambayo nimeziripoti polisi, wakatokomea navyo,
wakarusha pochi yangu chini, niliondoka pale na kuripoti polisi, na
Jalada la mashtaka tayari nimelifungua nasubiri haki intendeke,
Maswali ya kujiuliza,
Kwanza, ni kwanini mkurugenzi, mwenyekiti wa halmashauri bwFara,na madiwani wake ambao ni wajumbe wa Kikao hicho walitaka orodha hiyo iwe Siri wakati walijua imechakachuliwa ?
Pili kuna taratibu za kanuni za halmashauri zilivunjwa kwani Kikao hicho kilikuwa halali,na nyaraka hizo zilikuwa za vikao husika na siku zote kwa mujibu kwa kanuni tunapewa siku nne Kabla na baada ya Kikao kila Mjumbe a naondoka na kabrasha lake ,kwanini Leo wanawazuia wajumbe wasiondoke nazo?
Tatu JE mamlaka ya kunisachi mkoba wangu hususan wao wanaume na kunikaba na kunichania blauzi kifuani yaani , mkurugenzi na mkiti wa halmashauri wao wametoa wapi? Hata hivyo mie ni mbunge na ninadiplomatic passport, hata Uwanja wa ndege tu sisachiwi, JE wao wapo juu ya Sheria?
Mwisho ni dhahiri Kuwa mkurugenzi hajui wajibu wake ye Kama mtendaji mkuu wa halmashauri,na madiwani wa ccm wakiongozwa na mkiti wao wameshindwa kujibu hoja zangu ,hivyo wameanza kutumia mabavu.
0 comments:
Post a Comment