SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, June 9, 2012

AMREFwafanya tamasha la vijana kuhusu haki ya afya ya uzazi mjini iringa leo.

Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Meya wa Mkoa wa Iringa,Mh Gervas Ndaki akizungumza mapema leo mchana kwenye tamasha la Vijana kuhusu haki ya afya ya Uzazi,lenye kauli mbiu iliyohusu:MABADILIKO YANAANZA NA SISI,TIMIZA WAJIBU WAKO,TETEA HAKI YA AFYA YA UZAZI KWA VIJANA KATIKA NGAZI ZOTE.Tamasha hilo limeandaliwa na shirika la AMREF na kufanyika kwenye uwanja wa Mwembe Togwa,jijini Iringa ambapo wakazi mbalimbali wa mjini humo walijitokeza kupata elimu mbalimbali kuhusiana na afya ya uzazi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa,Bi.Theresia Mahongo akizungumza mapema leo mchana kwenye tamasha la Vijana kuhusu haki ya afya ya Uzazi,lenye kauli mbiu iliyohusu:MABADILIKO YANAANZA NA SISI,TIMIZA WAJIBU WAKO,TETEA HAKI YA AFYA YA UZAZI KWA VIJANA KATIKA NGAZI ZOTE.Tamasha hilo limeandaliwa na shirika la AMREF na kufanyika kwenye uwanja wa Mwembe Togwa,jijini Iringa ambapo wakazi mbalimbali wa mjini humo walijitokeza kupata elimu mbalimbali kuhusiana na afya ya uzazi.
Pichani ni Afisa Utetetezi   na sera kwa niaba  Meneja wa mradi wa haki ya afya ya uzazi  kwa vijana,Bw.Meshack Mollel akizungumza mapema leo kwenye tamasha la Vijana kuhusu haki ya afya ya Uzazi,lilioandaliwa na shirika la AMREF na kufanyika kwenye uwanja wa Mwembe Togwa,jijini Iringa ambapo wakazi mbalimbali wa Iringa walijitokeza kupata elimu mbalimbali kuhusiana na afya ya uzazi.
Pichani wa tatu kulia ni John Ambrose kutoka (APCS) wakiwa katika kundi la pamoja lililohusiana na mambo ya Saikolojia ya jamii,lililoandaliwa na shirika la AMREF,ambalo limefanyika kwenye tamasha la Vijana kuhusu haki ya afya ya Uzazi
Baadhi ya wasanii wa kikundi cha maigizo na ngoma za utamaduni kiitwacho Mzizi Cultural Troup chenye makazi yake mkoani Iringa,wakiigiza kwenye tamasha la Vijana kuhusu haki ya afya ya Uzazi ambalo limefanyika leo kwenye uwanja wa Mwembe Togwa mjini Iringa.
Baadhi ya wasanii wa kikundi cha maigizo na ngoma za utamaduni kiitwacho Mzizi Cultural Troup chenye makazi yake mkoani Iringa,wakiionesha umahiri wao wa kucheza goma za kiasilia kwenye tamasha la Vijana kuhusu haki ya afya ya Uzazi, ambalo limefanyika leo kwenye uwanja wa Mwembe Togwa mjini Iringa.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule mbalimbali waliofika kwenye tamasha hilo na kujisomea majarida mbalimbali yaliyohusu haki ya afya ya Uzazi na mambo mengineyo,ndani ya uwanja wa Mwembe Togwa mjini Iringa.
Baadhi ya Watoto wakijisomea vijarida mbalimbali vilivyohusu haki ya afya ya Uzazi na mambo menineyo,ndani ya uwanja wa Mwembe Togwa mjini Iringa.
Baadhi ya wakazi wa Mji wa Iringa waliojitokeza kwenye tamasha la Vijana kuhusu haki ya afya ya Uzazi,lenye kauli mbiu iliyohusu:MABADILIKO YANAANZA NA SISI,TIMIZA WAJIBU WAKO,TETEA HAKI YA AFYA YA UZAZI KWA VIJANA KATIKA NGAZI ZOTE.Tamasha hilo limeandaliwa na shirika la AMREF na kufanyika kwenye uwanja wa Mwembe Togwa,jijini Iringa ambapo wakazi mbalimbali wa mjini humo walijitokeza kupata elimu mbalimbali kuhusiana na afya ya uzazi.

0 comments:

Post a Comment