Mkuu
wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye
akimkabidhi mtoto Beatrice Phinius wa kituo cha watoto yatima Amani
Orphanage Centre cha Boko moja ya misaada iliyotolewa na wafanyakazi wa
benki hiyo kwa ajili ya watoto wa kituo hicho. Anayeshuhudia katikati ni
Mkurugenzi wa kituo hicho Margaret Mwegalawa.
Mkuu
wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye
na mfanyakazi wa benki hiyo tawi la Samora, Shose Kombe wakiwa
wamewabeba watoto yatima wanaolelewa na Kituo cha watoto yatima cha
Amani Orphanage Centre cha Boko jijini wakati wa hafla ya kukabidhi
msaada wa vyakula wenye thamani ya milioni 1.5/-.
Mkuu
wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye
(Kushoto) akiteta jambo na Afisa Mahusiano kwa Umma wa benki hiyo Gigi
Maajah mara baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi msaada kwa Kituo
cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre cha Boko jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya misaada iliyotolewa na KCB TANZANIA kwa kituo cha watoto yatima cha
Amani Orphanage Centre cha Boko jijini Dar es Salaam. Benki hiyo
ilikabidhi mchele, sukari, Unga wa Sembe, nguo za aina mbalimbali
zikiwemo shuka za kujifunika na kitanda cha mtoto mdogo vyote vikiwa na
thamani ya shilingi milioni 1.5/-.
Mkuu
wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye
akimkabidhi mtoto Jack Saguno wa kituo cha watoto yatima Amani Orphanage
Centre cha Boko moja ya misaada iliyotolewa na wafanyakazi wa benki
hiyo kwa ajili ya watoto wa kituo hicho. Anayeshuhudia katikati ni
Mkurugenzi wa kituo hicho Margaret Mwegalawa.
Watoto
yatima wa kituo cha Amani Orphanage Centre cha Boko jijini
wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania
Christine Manyenye (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi msaada
uliotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo wenye thamani ya milioni 1.5 kwa
watoto 60 wanaolelewa kituoni hapo.
Habari zaidi:
0 comments:
Post a Comment