ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A LOWEST COST AND ALSO SEND TO US NEWS, EVENTS FOR MORE INFORMATION CONTACT US TELEPHONE: +919160901191 E-mail: ally.shaaban@yahoo.com | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU NA PIA TUTUMIE HABARI, MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +919160901191 Barua Pepe: ally.shaaban@yahoo.com | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI HAPA

Saturday, October 30, 2010

Ivory Coast kuandaa uchaguzi mkuu kesho
Rais wa Ivory Coast
Raia wa Ivory Coast wanajianda kwa uchaguzi mkuu utakaoandaliwa hapo kesho, uchaguzi ambao ni wa kwanza kwa zaidi ya miaka 10.
Inatarajiwa kuwa uchaguzi huo mkuu utaunganisha tena taifa hilo ambalo liligawanyika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002.
Tangu wakati huo sehemu kadhaa za taifa hilo zimekuwa chini ya uthibiti wa makundi ya waasi.
Rais wa sasa Laurent Gbagbo, atapambana na rais wa zamana wa nchi hiyo Henri Konan Bedie, ambaye aliondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi mwaka 1999.
Mgombeaji mwingine ni Alassane Outtara ambaye hakushiriki katika uchaguzi zilizopita kwa kuwa alituhumiwa kuwa raia wa kigeni.
Wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanasema uchaguzi huo utakuwa mgumu na huenda asipatikane mshindi wa moja kwa moja.
Vile vile wanaonya kuwa huenda ghasia zikashuhudiwa nchini humo ikiwa matokeo ya uchaguzi wa urais yatakuwa na utata
Uchaguzi mkuu kufanyika kesho Tanzania
Raia wa Tanzania wanajiandaa kwa uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika hapo kesho.
Wafuasi wa chama cha CCM
Wafuasi wa chama cha CCM
Vyama vya kisiasa vinatarajiwa kukamilisha kampeini zao hii leo.
Wafuasi wa rais wa nchi hiyo, Jakaya Kikwete wanatarajiwa kufika jijini Dar es Salaam, kuhudhuria mkutano wa mwisho wa kampeini,wa chama tawala cha CCM.
Kuna ushindani mkali katika kinyanganyiro cha kuwania kiti cha urais.
Miongoni mwa watu wanaowania kiti hicho ni pamoja na rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye alizoa asilimia 85 ya kura zote zilizopigwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete
Wakosoaji wa Rais Kikwete wanasema ameshindwa kukabiliana na ufisadi na kuhakikisha kuwa rasilimali ya nchi inawafikia raia wa Kawaida.
Rais Kikwete atapamabana wapinzani wengine akiwemo Willibrod Slaa ambaye ameahaidi kupambana na ufisadi na kuanzisha huduma za afya na elimu bila malipo nchini humo endapo atachaguliwa kuongoza taifa hilo.
Mwingine ni Ibrahim Lipumba ambaye amehaidi kubuni serikali ya muungano wa kitaifa ili kutatua matatizo ya taifa hilo ikiwa atashinda uchaguzi huo.
Wapiga kura milioni 19.6 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hilo.


Tunamuomba M/Mungu ajaalie Uchaguzi huu ufanyike mwanzo hadi mwisho uwe wa Haki na Huru, Salama na Amani.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Amin.
JK ajibu maswali LIVE kwenye TV jana usiku!
Usiku wa jana mgombea urais kwa tiketi ya ccm, Dk, Jakaya Mrisho Kikwete, ameongea na vyombo vya habari vya televisheni, ITV, Channel Ten, TBC1, ATN, Mlimani TV, Star TV na Clouds TV na kuulizwa maswali kadhaa, yakiwemo haya yafuatayo na majibu yake:


TAFITI ZA SYNOVET NA REDET
CCM haina uhusiano na kampuni hizo za utafiti. Synovate wanalipwa na wazungu, Redet pia wanalipwa na wazungu. Sisi pia hatukubaliani na tafiti zao, hatukubaliani na asilimia 61 ya Synovate wala 71 ya Redet, tunaamini tutapata zaidi ya hapo.
Ccm haichakachui matokeo, wanaochakachua mnawajua. Mmeona nao wameanzanisha ya kwao, ambapo baadhi ya viongozi wao wa chama ndiyo wamiliki wa hiyo kampuni ya utafiti…..kicheko…

SUALA LA JIRA KWA VIJANA 
Ukosefu wa ajira ni ‘time bomb’ , lengo limevukwa kwa kuwa na ajira mil 1.3 badala ya mil 1. Hata hivyo mafanikio hayo ni sawa na toni la maji baharini. Bado kuna tatizo la ajira. Tunahitaji wawekezaji ili kupata ajira zaidi na haiwezekani kuwakataa wawekezaji tukawa na ajira. Siri ya ajira ni uwekezaji, hata kama ni mdogo kiasi gani.

SURA YA SERIKALI IJAYO 
Dhamira yangu Kubwa ni kuona tunatumia teknolojia ya mawasiliano zaidi na kuondoa ile tabia ya kufanya jambo lazima ukamuone mtu. Mfano kuomba passport na leseni ya biashara muomboji hatolazimika kumuona ofisa na pia rushwa itapungua.
Pia ifikapo Juni 2011, Wilaya zote zitaunganishwa kwenye mtandao kupitia mkonga wa mawasiliano wa fibre optic. Hivyo sura ya serikali ijayo ni ya e-goverment ambayo itaunganisha wizara zote kwenye mtandao.

UTAPENDA WATANZANIA WAKUKUMBUKE KWA LIPI UKIPATA NAFASI YA KUONGOZA KWA MIAKA MITANO TENA NA KUIMALIZA (LEGACY)
Watanzania wanikubuke kwamba ‘niliwakuta hapa, nimewaacha hapa’ basi! Niliwakuta wakiwa hali ya chini na nimeondoka wakiwa na nafuu. Hii ikiwa ni katika kila sekta zote, barabara, elimu, afya, n.k.

VITAMBULISHO VYA URAIA VP? HILO LIMEKWAMA WAPI NA KAMA HALIJAKWAMA LIMEFIKA WAPI?
Ni kweli kwamba ahadi ya vitambulisho ni ya muda mrefu, siyo la awamu hii tu. Bahati mbaya sana ni mradi ambao umepitia misukosuko mingi na imechangiwa na migongano ya kimaslahi ya watu binafsi. Hata hivyo baada ya muda atapatikana mtu wa kufanyakazi hiyo, katika miaka miwili ijayo vitakuwa vimetoka au vitakuwa vimeenza kutoka.

SEKTA YA MADINI SERIKALI IMECHUKUA HATUA GANI BAADA YA KUUNDA KAMATI?
Tumetengeneza sera na sheria mpya ya Madani. Tumerekebisha viwango vya mrabaha, kuna maeneo tumeongeza na maeneo mengine tumepunguza. Una manufaa ya pande zote. Wa Mwanzo ulikuwa umetulalia sisi, lakini sasa mchango wa Madini umeanza kutoa mchango mkubwa wa mapato. Kwa mwaka huu umeingiza zaidi ya dola milioni 4.5

WATU WENGI WANAPELEKWA NJE KWA MATIBABU!
Tunalazimika kupeleka watu wetu nje kwa sababu bado baadhi ya mardhi hatuna uwezo wa kuyatibu. Tunapeleka watu nje kwa sababu hatuna wataalamu au vifaa vya kutibu maradhi hayo. Katika kipindi hiki, tumefundisha madaktari wapatao 265 kutoka 46.
Tumejenga pale Muhimbili kitengo cha kutibu magonjwa ya kinywa ambacho ni bora kuliko vyote Afrika Mashariki na kati. 
Pia tumeshaweka jiwe la msingi katika hospitali ya Muhimbili la kujenga kitengo cha kutibu magonjwa ya moyo (open surgery) ambacho kitakuwa na vitanda 100.
Tumejenga mashine ya kusafisha figo Muhimbili, ambayo ina vifaa vyote vya kisasa (complete equipment), hii yote ni kuhakikisha tunakuwa na uwezo wa kutibu magonjwa mengi hapa hapa nchini.
Pia kitengo cha MOI kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya upasuaji wa misuli kuanzaia mwakani.

MUUNGANO: KUNA TATIZO LA MUUNGANO, UNAWEZA KUTUPA SURA YA SERIKALI YA MUUNGANO INAYOKUJA ILI KUONDOA MALALAMIKO.
NI kweli kila wakati kuna maswali yanaibuka kuhusu muungano. Lakini kuna kamati maalum imeundwa kushughulikia suala la muungano na matatizo mengi yameshatatuliwa na kuna masuala mengi tumekubaliana. Masuala yaliyobaki kujadiliwa ni machache ambayo katika kipindi kijacho yote tutakuwa tumeyapatia majibu.

UMETOA AHADI NYINGI SANA NA TAMU SANA, JE AHADI HIZI ZITATEKELZWA VP?
Kwanza kuna ilani za chama na kuna ahadi za papo kwa papo. Katika awamu ya kwanza mara baada ya cunda serikali, nilikutana na mawaziri wote, nikawapa ilani na kuwataka kuandaa mpango wa utekelezaji wa ilani zilizotolewa na nyingi zimetekelezwa. Tunakutoa wasiwasi, mengi ya haya tunayoyaahidi tutayatekeleza.

UTASHUGHULIKIA VP SUALA LA RUSHWA
Kwanza tumetunga sheria ya kupambana na rushwa na baada ya hapo tumejenga taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, TAKUKURU, tumeiongezea uwezo. Kwa kufanya hivyo matokeo yake tumeyaona, wameweza kuwafikisha watu wengi mahakamani. Lakini tatizo la rushwa ni Kubwa hata katika vitabu vya dini limetajwa. Nawaahidi tutaendelea kupambana nalo.

MANUNG’UNIKO DHIDI YA MAHAKAMA
Tumeanza kujenga mfumo wa kisasa wa kusikiliza kesi ambapo mienendo yake itakuwa ikirekodiwa kama hansard. Pia tumeongeza majaji, kuna tatizo la maadili kwa watendaji, hili tunaomba tushirikiane kulitatua.

MWISHO
RAI YA RAIS: TUENDELEE KUDUMISHA AMANI, TUHESHIMU MATOKEO. TUMIENI KURA ZENU KUMCHAGUA MNAYEMTAKA. TUSICHAGUANE KWA MISNGI YA DINI. VYOMBO VYA HABARI VIACHE KUCHOCHEA MAMBO.
chanzo http://www.globalpublishers.info/

Friday, October 29, 2010

Courtside Shots: Justin Bieber & Jaden Smith Watch the Lakers Take on the Rockets in Los Angeles
Courtside Shots: Justin Bieber & David Beckam.

ALI KIBA NDANI YA CHICAGO

Ali Kiba (kulia) akiwa na 2Face Idibia wakipitia mistari.

Ali Kiba (wa nne kushoto) akiwa pamoja na wasanii wenzake ndani ya Chicago.

Ali Kiba 2Face na Jk.
Ali Kiba akiwa ndani ya Saloon.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA HAKI NGOWI

Mwenyekiti wa AU: Afrika inapaswa kupigania ruzuku za kilimo

Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi ambaye ni Mwenyekiti wa kiduru wa Umoja wa Afrika AU amesema kuwa bara la Afrika linapaswa kupigania ruzuku za wakulima masikini ili bara hilo liwe na usalama wa chakula. Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa IMF zimezuia ruzuku za kilimo kwa wakulima masikini wa Kiafrika kutokana na gharama kubwa ya ruzuku hizo. Mutharika amesisitiza kwamba, nchi za Kiafrika zinapaswa kusimama kidete na kupigania ruzuku hizo za wakulima masikini, na kwamba uanachama mpya na jumuiya za utoaji misaada unapaswa kuwepo kwa kuzingatia uimarishaji ruzuku kwa wakulima wanaomiliki mashamba madogo hasa wanawake. Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika aidha ameongeza kuwa, haiyumkiniki wakulima wa Kiafrika kuweza kulima bila kupewa ruzuku, kwani ruzuku hiyo huelekezwa moja kwa moja katika ununuaji mbolea, mbegu, dawa za kuulia vijidudu, matrekta, vifaa vya umwagiliaji na huduma nyinginezo.
Mwapachu: EAC haitoweza kusaini makubaliano ya kibiashara na EU Novemba
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema kuwa jumuiya hiyo haitoweza kutia saini makubaliano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya katika muda uliopangwa ambao ni mwezi Novemba. Juma Mwapachu aidha ameelezea matumaini yake kwamba makubaliano mengine yatafikiwa kuhusiana na ushirikiano wa kiuchumi, ambayo yameandaliwa ili kuchukua nafasi ya makubaliano ya kibiashara yanayoonekana kuwa na upendeleo yaliyokwamishwa na Shirika la Biashara Duniani (WTO). 

Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mshariki EAC ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi zenye jumla ya pato linalotokana na uzalishaji wa ndani la bilioni 73.3, kwa miezi kadhaa sasa zinajitayarisha kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya, baada ya kuanzisha makubaliano ya EPA mwaka 2007 na kudhamini kujiunga kwao na masoko ya Ulaya. 
Misri yawakandamiza wapinzani na kukataa wasimamizi wa nje
Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imeelezea wasiwasi wake kuhusiana na vitendo vinavyoongezeka vya serikali vya kuwakandamiza wafuasi wake, kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao. Mohammed Badie Kiongozi wa harakati hiyo ametoa matamshi hayo huku polisi ya Misri ikiwa mpaka sasa imewakamata zaidi ya wafuasi 250 wa harakati hiyo mwezi huu. Ikhwanul Muslimin inahesabiwa kuwa ni chama cha upinzani chenye nguvu na tishio kwa chama tawala katika uchaguzi ujao wa bunge nchini humo.

Wakati hayo yakiripotiwa, chama tawala cha Misri kimekataa kuwepo aina yoyote ya wasimamizi kutoka nje ya nchi katika uchaguzi ujao wa bunge wa nchi hiyo. Zakaria Azami Naibu Katibu wa chama hicho anayesimamia masuala ya fedha na ya kiidara amesema kuwa, chama hicho hakikubaliani na kuwepo aina yoyote ya usimamizi wa kimataifa katika uchaguzi wa bunge na hivi karibuni kitatangaza rasmi wagombea wake.
chanzo  http://kiswahili.irib.ir/
Misaada yawasili Indonesia
Mkaazi wa kisiwa cha Mentawai magahribi mwa Sumatra
Mkaazi wa kisiwa cha Mentawai magahribi mwa Sumatra
Misaada imeendelea kuwafikia wale waliokumbwa na maafa Indonesia baada ya meli tatu kufika katika kisiwa kilichoharibiwa zaidi na tsunami.
Vikosi vya uokoaji sasa wanajitahidi kusaidia watu katika kisiwa cha Pagai Kaskazini magharibi mwa Sumatra.
Inafahamika kuwa zaidi ya watu 340 wamefariki dunia.Mamia bado hawajulikani walipo.
Rais wa Indonesia
Rais wa Indonesia ametembelea visiwa hivyo.
Rais Susilo Bambang Yudhoyono alikatiza safari yake huko Vietnam ili kusimamia shughuli ya uokoaji,na alisafiri kwa helikopta ambayo ilikuwa imebeba vyakula na bidhaa zengine muhimu.
Huko alikutana na wale walionusurika pamoja na viongozi wa eneo hilo.
Ameahidi kuwa serikali itasaidia utawala wa Sumatra Magharibi kujenga nyumba za muda, vituo vya afya na shule, msemaji wake alisema.
Msaada huo umefika huku Indonesia ikikabiliana na maafa mengine yaliyoletwa na mlipuko wa mlima Merapi katikati mwa Java.
EU kudhibiti msukosuko wa kifedha
Euro
Euro
Viongozi wa muungano wa Ulaya wamekubaliana kuhusu mpango wa kudumu utakaolinda muungano huo kutoka na msukosuko wa kifedha.
Pia wamekubaliana kuwa na mbinu moja itakayokokabiliana na nchi yeyote itakayotishia udhibiti wa sarafu moja kama Ugiriki mapema mwaka huu.
Viongozi hao wamekubaliana kuimarisha udhibiti katika nchi zinazotumia sarafu ya euro. Hatua hiyo itauwezesha muungano huo kuchunguza bajeti za nchi wanachama,kutoa ushauri kuhusu mipango ya kibiashara ambayo huenda ikaleta hasara,kutoza faini nchi zinazoomba mikopo na kutumia fedha nyingi.
Mpango huo utarahisisha utekelezaji wa hatua kama hizo.
Ni mpango unaonuiwa kulazimisha nchi wanachama, kusuluhisha matatizo yao ya kifedha kabla matatizo hayo kuanza kutishia nchi zingine zinamazotumia sarafu ya euro.
Pia utakuwa na mfuko wa dharura utakaochukua nafasi ya ule wa muda uliowekwa ili kukwamua nchi ya Ugiriki.
Lakini kwa hilo kufanyika Ujerumani inasisitiza kuwa ni lazima mkataba wa Lisbon ufanyiwe marekebisho.
Rais wa baraza la Muungano wa Ulaya Herman Van Rumpey, amepewa kazi ya kuangalia jinsi hilo litakavyowezekana bila kubadilisha mkataba wa Lisbon katika nchi zote 27.

Thursday, October 28, 2010

DK. KIKWETE AUNGURUMA KIWALANI
MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Jakaya Mrisho Kikwete leo ameongea na wananchi wa jimbo la Segerea Kata ya Kiwalani jijini Dar es Salaam zikiwa zimebaki siku tatu kufikia siku ya uchaguzi mkuu. Ziara hiyo ilitarajiwa kuendelea huko Ukonga na kumalizikia katika viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke. Pichani ni sehemu ya umati uliohudhuria mkutano wa Kiwalani.
..wakimsiliza JK kwa makini licha ya jua kali
JK akisalimiana na wananchi wakati akiwasili Kiwalani leo
Mwanadada na taswira ya mkutanoni Kiwalani leo

ZIKIWA ZIMEBAKIA SIKU KADHAA KARATASI ZA KURA ZAWASILI PEMBA CHINI YA ULINZI MKALI

Karatasi za kupigia kura zawasili kisiwani pemba na ndege ya ZanAir zikitokea Zanzibar tayari kwa uchaguzi siku ya Jumapili Oktoba 31
Magari ya Tume yakisubiri kupokea karatasi
Baadhi ya maafisa waandamizi wakishuhudia kuwasili kwa karatasi za kura
Mzigo ukishushwa kutoka katika ndege ya Zan Air
Ukisubiri kupakiwa kwenye magari
Hapa wahusika wanaonekana wakielekezana jambo fulani muhimu

Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi kutoka nje na ndani ya nchi walikuwepo kushuhudia
Karatasi za kura zikiondoka uwanja wa ndege
Picha na Mussa Bakar Pemba

Tsunami Indonesia:Waliokufa sasa ni 282

Idadi ya waliofariki dunia kufwatia tsunami katika visiwa vya nchini Indonesia imeongezeka hadi 282,maafisa wamesema.
Vikosi vya uokoaji katika visiwa vya Mentawai wanasema mamia ya watu bado hawajulikani walipo,siku mbili baada tetemeko la ardhi kusababisha tsunami magharibi mwa Sumatra.
Maafisa wanasema kulikuwa na matatizo katika mtambo uliotengenezwa kwa lengo la kutoa tahadhari kwa wakaazi juu ya kuzidi kwa mawimbi.
Rais wa Indonesia amekatiza ziara yake ya nchini Vietnam ili aweze kutembelea visiwa hivyo pamoja na kusimamia shughuli za uokozi.
Rais Susilo Bambang Yudhoyono anatarajiwa kuzuru eneo hilo siku ya alhamisi kutathmini juhudi za misaada.
Pia ataelezwa kuhusu uokoaji katika eneo la Java, ambapo mlipuko wa volcano umesababisha maafa

Waziri wa Mambo ya Nje Kenya ajiuzulu

Moses Wetangula
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Moses Wetangula amejiuzulu ili kutoa nafasi ya kufanywa uchunguzi kuhusiana na kashfa ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Kenya jijini Tokyo, Japan.
Mwingine aliyejiuzulu kufuatia kashfa hiyo ni katibu wa wizara ya mambo ya nje Thuita Mwangi.
Wote wanashutumiwa kukiuka mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu kuhusu gharama ya jengo hilo.
Kamati ya bunge kuhusu masuala ya nchi za nje na ulinzi, iliwasilisha taarifa bungeni ikipendekeza waziri Moses Wetangula na katibu huyo wajiuzulu, kufuatia sakata hiyo inayokisiwa kuigharimu serikali ya Kenya dola milioni 13.5. Pia kumekuwa na kashfa ya kupotea fedha katika ubalozi wa Kenya ncini Misri, Nigeria, Pakistan na Ubelgiji
Siku ya Jumanne kulikuwa na mjadala mkali ndani ya Bunge la Kenya kuhusiana na ripoti hiyo.
Bw Wetangula amekanusha tuhuma zote hizo. Tuhuma za hivi sasa za ufisadi ndio zinaonekana nzito kugusa kiongozi mwenye dhamana kubwa serikalini mwandamizi.

Wednesday, October 27, 2010

ALI KIBA NA MPANGO WA ONE8
Ali kiba akiwa na wenzake wa ONE8 group wakiredi single yao pande za chi-town USA

Man Utd Hero Javier Hernandez earns Ferguson Praise
Sir Alex Ferguson heaped further praise on Javier Hernandez after his 90th minute winner propelled Manchester United into the quarter-finals of the Carling Cup on Tuesday night.
The Mexico international was the United hero for the second time in as many days after he came off the bench to sink Wolves at Old 
Trafford.Hernandez, who scored twice at Stoke on Sunday, stepped off the bench to give United a 3-2 victory at home to Wolves.
JK AWANADI MASHA NA DIALLO MWANZA
JK akimnadi mgombe ubunge wa CCM jimbo la Nyamagana Mh. Lau Masha jana jioni.

JK akimnadi mgombea ubunge wa CCM jimbo la Ilemera Mh. Anthony Diallo kwenye mkutano wa kampeni wa Mh. Lau Masha katika uwanja wa Sahara ambapo Mh. Diallo aliwafagilia sana JK na mgombea huyo wa Nyamagana jana.
JK akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Sehemu ya maelfu ya wananchi wa Mwanza mkutanoni hapo jana.
DK SLAA AFUNIKA MANZESE NA MWEMBE YANGA DAR
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, katika mkutano wa kampeni, kwenye Uwanja wa MwembeYanga, Temeke jana jioni.

Wapenzi na wananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwa na bango lenye ujumbe mbalimbali, katika mkutano wa mgombea urais kupitia chama hicho, Dk.
Willibrod Slaa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke
jijini Dar es Salaam jana jioni.


Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wakazi wa Manzese jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake wa kampeni jana mchana.
Picha kwa hisani ya Joseph Senga wa Tanzania Daima.
"KUBALINI MATOKEO, MSIPORIDHIKA FUATENI SHERIA"
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Said Mwema.

SERIKALI kupitia vikosi vya ulinzi na usalama, imetoa tahadhari kwa waliojipanga kuyakataa matokeo ya uchaguzi, wajiepushe na uvunjifu wa amani na kama hawatoridhika na matokeo hayo, wadai haki yao kwa kufuata sheria na kanuni zilizopo.

Aidha, ili kuwahakikishia amani na utulivu Watanzania katika siku chache zilizobakia za kampeni na baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi, Jeshi la Polisi limetangaza kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Magereza na Mgambo.

Uthibitisho huo wa utulivu na amani wakati wa uchaguzi, umetolewa jana kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Said Mwema na viongozi wengine wa serikali.
“Endapo matokeo yaliyotangazwa hayatokidhi matarajio ya mtu au kikundi chochote, ni vyema utaratibu wa kisheria ukafuatwa pasipo uvunjifu wa sheria,” alisema Mwema.
Alisema, ingawa wajibu wa usalama na amani pia ni wa wananchi, Polisi imejipanga kuhakikisha mikutano ya kampeni iliyobakia inamalizika kwa usalama, utaratibu wa kupiga kura unafanyika kwa amani na utulivu na vifaa vya kupigia kura vinalindwa ili visiibiwe, visitekwe wala kughushiwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, alisema mchakato wa uchaguzi umekuwa shwari isipokuwa kuna matukio kadhaa yaliyotia dosari.
Aliyataja matukio hayo kuwa ni kuchana mabango ya wagombea, lugha chafu na wanachama wa vyama tofauti kushambuliana na kutoa taarifa za uvumi kwa njia ya simu na mtandao.
Masha ambaye alitoa taarifa yake mkoani Mwanza alisema: Wananchi wote wa Tanzania watapiga kura kwa amani na utulivu Oktoba 31 na wale watakaoleta vurugu, neno langu ni moja kwao ya kuwa wawe tayari kuvuna walichokipanda.”
Alisema, Serikali inawashukuru Watanzania kwa kuonesha ukomavu wa kisiasa katika kampeni na kuhakikisha hakuna mtu aliyepoteza maisha hadi wakati huu.
“Lakini kule Shinyanga mwanachama mmoja wa CCM kwa sababu tu alikutwa ameweka bango la CCM tayari ameuawa hivi tunaelekea wap?”
Alihoji na kuvitaka vyama vya siasa viongozi wao na wananchi kwa ujumla kuheshimu taratibu za uchaguzi.
Alisema serikali haimzuii mtu yeyote kufanya ushabiki ndani ya chama anachokipenda, lakini akasisitiza kuwa ushabiki huo sharti uzingatie sheria na utaratibu.
Chanzo http://www.globalpublishers.info/
Tsunami yaua watu wengi Indonesia
Kipigo cha tsunami
Kipigo cha tsunami

Zaidi ya watu 100 wameuawa na wengine wengi hawajulikani walipo kufwatia tsunami iliyosababishwa na tetemeko la ardhi katika pwani ya Sumatra nchini Indonesia.
Maafisa wanaoshugulika na misaada pia wanajaribu kukabiliana na athari za mlipuko wa volkeno katika Mlima Merapi Katikati mwa Java.Nyumba kadhaa ziliharibiwa na mawimbi ya bahari karibu na visiwa vya Mentawai.
Maji yaliyofurika yaliharibu kabisa vijiji kumi kwenye visiwa hivyo, afisa mmoja anayeshughulika na uokoaji aliambia shirika la habari la AFP.
Baadhi ya watu walioachwa bila makao
Hali mbaya ya hewa na uharibifu imechelewesha juhudi za kufikia maeneo yaliyoathirika.
Hendri Dori Satoko,mjumbe katika visiwa vya Mentawai,aliambia kituo cha televisheni cha Metro: "takwimu zetu za hivi punde zinaonyesha kuwa watu 108 wameuawa na wengine 502 hawajulikani walipo."
Alisema baadhi ya wale ambapo hawajulikani walipo huenda walikimbilia maeneo salama ya juu na wanaogopa kurudi nyumbani kwao.
Maafisa wa wizara ya afya wanasema miili 113 imepatikana katika eneo hilo kufikia sasa,shirika la habari la Associated Press limeripoti.
Wakati huohuo maafisa wanasema zaidi ya watu elfu kumi na tatu wamehamishwa kutoka maeneo ya karibu na Mlima Merapi na kupelekwa katika kambi tangu mlipuko wa volkeno kutokea.
Lakini hali imeelezewa kuwa ngumu kutokana na idadi kubwa ya watu wanaotaka kuhama na kutafuta hifadhi katika maeneo salama.
Wakaazi wengi wa vijiji vilivyo karibu walipuuza onyo lililotolewa hapo awali na maafisa na hawakuwa tayari kuondoka na kuacha makao na mashamba yao.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUSOMA HABARI ZILIZOPITA BOFYA NENO OLDER POSTS HAPO JUU ASANTE SANA KWA KUTEMBELEA NA KARIBU TENA